Lakers wanuia kuingia nafasi za mchujo kwa kuishinda Pelicans


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 National Basketball Association (NBA) season

Regular Season

New Orleans Pelicans v Los Angeles Lakers 

Smoothie King Center 
New Orleans, USA
Monday, 28 March 2022
02h00  
 
New Orleans Pelicans watamenyana na Los Angeles Lakers katika mechi ya NBA mnamo Machi 28.
 
Mechi hii itakuwa ya 66 baina ya timu hizi katika msimu wa NBA tangu mwaka 2002, Pelicans ilivyoanzishwa.
 
The Lakers wamekuwa wababe katika mechi baina ya timu hizi mbili huku wakiandikisha ushindi mara 41 dhidi ya 24 kwa faida ya Pelicans.

Zion Williamson
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Mchuano wa mwisho baina ya Lakers na Pelicans ulikuwa Februari 28 2022 na ulichezewa katika ukumbi wa Crypto.com Arena, Los Angeles.
 
The Pelicans waliwazidi nguvu Lakers na kuibuka na ushindi wa 123-95 katika mechi iliyoshuhudia CJ McCollum akitia wavuni vikapu 22 kwa faida ya The New Orleans.
 
Pelicans wanakalia nafasi ya 10 katika jedwali la Western Conference baada ya kuandikisha ushindi mara 30 na kushindwa mara 42 katika mechi 72.
 
Kwa upande mwingine, Lakers wapo kwenye nafasi ya tisa vile vile katika jedwali la Western Conference baada ya kushinda mechi 31 na kushindwa mechi 41 katika mechi 72.

Lebron James
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Mchezaji nyota wa Lakers LeBron James alimpiku Karl Malone kama mfungaji bora wa pili katika historia ya NBA kwenye mechi waliyocheza na Washington Wizards Jumamosi.
 
James alimpiku Malone, mchezaji wa zamani wa Utah Jazz aliyeingia katika vitabu vya kumbukumbu kwa kufunga vikapu 36,928 kunako dakika ya 5:20 katika robo ya pili.
 
"Kuwa mchezaji wa ligi hii kwa miaka mingi niliyoshiriki,” alisema James alipoulizwa kuhusu mafanikio yake.
 
"Na kufananishwa na baadhi ya wachezaji waliowahi kucheza mchezo huu, wachezaji niliowashuhudia au kujifunza kutoka kwao na kuwasoma na niliotamani kuiga mfano wao, nakosa maneno ya kuelezea.
 
"Ni heshima kubwa kwangu, familia yangu na marafiki na sehemu nilikozaliwa kwa kutengeneza kumbukumbu katika safari hii, ambayo ni sababu kuu ya kucheza mchezo huu.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho, NBA

Mechi - 5
Pelicans - 2
Lakers - 3
 

Bashiri Mpira wa Kikapu na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.




Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 

Published: 03/25/2022