Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Italian Serie A
Matchday 31
Juventus FC v Inter Milan
Allianz Stadium
Torino, Italy
Sunday, 3 April 2022
Kick-off is at 21h45
Juventus FC na Inter Milan watamenyana katika
mechi ya ligi kuu nchini Italia ugani Allianz Stadium mnamo Aprili 3.
Katika mechi iliyopita ya Machi 20, Juventus wakiwa ugenini walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya US Salernitana
Kwa sasa Juventus wameshinda mechi 11 na kupata sare katika mechi tano kwenye mechi kumi na sita zilizopita za ligi.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Vile vile, The Old Lady hajashindwa katika mechi nane za ligi zilizopita akiwa nyumbani baada ya kuandikisha ushindi mara sita na kupata sare mbili.
"Tulishambulia vizuri. Kulikuwa na wasiwasi kuondolewa kwenye mechi za UEFA kutatuathiri kwa sababu wengi hawakutarajia tutolewe Jumanne,” alisema meneja wa Juventus Massimiliano Allegri baada ya ushindi dhidi ya Salernitana.
"Wachezaji walionyesha hari na kucheza vizuri. Tungefunga goli la tatu kipindi cha pili lakini uchovu ulituingia. Cha msingi ilikuwa ushindi na kupanua nafasi baina yetu na wanaotufuata.
"Inter wana mchezo mmoja zaidi yetu lakini kwa sasa tunazingatia mechi hii. Utakuwa mchezo mzuri pia kwa sababu wachezaji watakuwa wamepumzika."
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kwengineko, Inter wakiwa uga wa nyumbani walitoka sare ya 1-1 dhidi ya ACF Fiorentina katika mechi ya ligi iliyochezwa Machi 19.
Kwa sasa, Inter hawajashindwa katika mechi nne za ligi zilizopita huku wakiandikisha sare tatu na kushinda mechi moja.
Vile vile, hawajashindwa katika mechi tisa zilizopita za ligi wakiwa ugenini baada ya kuandikisha sare tano na ushindi mara nne.
Juventus na Inter walikutana mara ya mwisho katika mechi ya ligi tarehe 24 Oktoba 2021.
Timu hizo zilitoka sare ya 1-1 katika mechi hiyo iliyochezewa uwanja wa Stadio Giuseppe Meazza, maarufu kama San Siro.
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi
Mechi - 5
Juventus - 3
Inter - 1
Sare - 1
Ratiba ya Serie A, mechi ya 31
Jumamosi, Aprili 2
4:00pm - Spezia Calcio v Venezia FC
7:00pm - SS Lazio v US Sassuolo
9:45pm - US Salernitana v Torino FC
Jumamosi, Aprili 3
13:30pm - ACF Fiorentina v Empoli FC
4:00pm - Atalanta BC v SSC Napoli
4:00pm - Udinese Calcio v Cagliari
7:00pm - UC Sampdoria v AS Roma
9:45pm - Juventus FC v Inter Milan
Jumatatu, Aprili 4
7:30pm - Hellas Verona v Genoa CFC
9:25pm - AC Milan v Bologna FC
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.