City na United kucheza katika debi ya 187


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 English Premier League

Matchday 28

Manchester City v Manchester United

Etihad Stadium
Manchester, England
Sunday, 6 March 2022
Kick-off is at 19h30  
 
Machi 6 Jumapili, Manchester City wataialika Manchester United ugani Etihad kwenye mchezo wa ligi, na ambao utakuwa ni debi ya 187 baina ya timu hizi.
 
The Citizens wamekuwa viwango vya juu katika ligi muongo uliopita huku wakishinda taji la premier mara tano ukilinganisha na mara moja kwa faida ya The Red Devils.
 
Hata hivyo, City wameshinda mechi nne tu dhidi ya United katika mechi kumi zilizopita.
 
Mabingwa hao watetezi wanaongoza ligi kwa alama sita dhidi ya mpinzani wa karibu Liverpool huku wakiwa wamecheza mchezo mmoja zaidi.
 
Walijizoa baada ya kupoteza mechi dhidi ya Tottenham 3-2 Februari 19 na kushinda Everton 1-0 wikendi iliyopita.

Pep Guardiola
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Goli la City dhidi ya Everton lilipatikana dakika ya 82 baada ya mchezo mkali na Guardiola amekiri kuwa mechi zote zilizobaki zitakuwa ngumu kwao huku wakitazamia kuhifadhi taji.
 
"Ukweli ni kuwa kila mchezo utakuwa kama wa leo dhidi ya Everton,” Guardiola alisema baada ya mechi dhidi ya Everton. “Kila timu ina malengo yake; kutoshushwa daraja, kucheza Europa, kucheza ligi ya mabingwa na kuwa mabingwa.  
 
"Kila mechi itakuwa ngumu na tumeshalizungumzia hilo. Sio mara ya kwanza kuwa katika hali na tutajifunza kutoka tuliyoyapitia hapo mbeleni.
 
"Iwapo unataka kuwa bingwa dhidi ya mpinzani kama Liverpool, ni sharti ushinde mechi zako kwa sababu itakuwa vigumu kwa Liverpool kupoteza michezo.”
 
United walipoteza alama zaidi na ndoto yao ya kumaliza nne bora kuingia doa baada ya kutoa sare katika mechi dhidi ya Watford Jumamosi iliyopita ugani Old Trafford.
 
Ralf Rangnick amepoteza mechi moja tu ya ligi tangu alipoiridhi mikoba ya Ole na timu hiyo haijapoteza mechi kati ya michezo minane iliyocheza.
 
Wanabakia katika nafasi ya nne, alama mbili zaidi ya West Ham ingawaje wote wamecheza mechi tatu zaidi ya Arsenal walioko katika nafasi ya sita.

Ralf Rangnick
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Rangnick alishuhudia nafasi nyingine ikipotea na kukiri kuwa timu yake haiwezi kuendelea kupoteza alama zaidi ikiwa wanataka kufuzu kucheza UEFA Champions League.
 
"Tunahitaji kujituma zaidi ili kujiandaa kwa mchezo dhidi ya City Jumapili inayokuja lakini alama mbili tulizopoteza zinatuumiza,” alisema mjerumani huyo.
 
"Maandalizi dhidi ya City yataanza mwanzoni mwa wiki ijayo. Kwa sasa tunajiskia vibaya na kama nilivyosema awali, sio mara ya kwanza sisi kupoteza alama mbili muhimu.”
 

Takwimu baina ya timu hizi katika michezo 5 ya ligi iliyopita

 
Mechi - 5
Man City - 1
Man United - 3
Sare - 1

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 
 

Published: 03/03/2022