Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Spanish La Liga
Matchday 30
FC Barcelona v Sevilla FC
Camp Nou
Barcelona, Spain
Sunday, 3 April 2022
Kick-off is at 22h00
FC Barcelona na Sevilla FC watamenyana katika
mechi ya ligi kuu Uhispania ugani Camp Nou, Aprili 3.
Katika mechi ya ligi iliyochezwa Machi 20, Barcelona wakiwa ugenini Santiago Barnabeu waliishinda Real Madrid 4-0.
Barcelona hawajashindwa katika mechi 13 za ligi zilizopita huku wakiandikisha ushindi katika mechi 9 na kupata sare 4.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Vile vile, Barcelona wameandikisha ushindi mara nne mfululizo katika mechi nne za ligi walizocheza nyumbani Camp Nou.
"Nina raha nyingi. Ni jioni ya kupendeza. Hii ni Barcelona tunayoifahamu. Tumeonyesha uwezo wetu dhidi ya timu nzuri ya Real Madrid katika uwanja wao wa nyumbani,” alisema meneja wa Barcelona Xavi Hernandez.
"Ni mafanikio makubwa yatakayotupa matumaini katika kazi tunayofanya. Furaha yangu tulionyesha mchezo mzuri kuliko Madrid. Tulicheza vizuri sana.
"Nafurahia sana kwa sababu, licha ya kuwa kocha wa Barcelona, mimi pia ni shabiki mkubwa wa klabu hii. Huwezi kusahau jioni kama ya leo.”
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kwengineko, Sevilla walilazimisha sare ya 0-0 dhidi ya Real Sociedad wakiwa nyumbani katika mechi ya ligi ya tarehe 20 Machi.
Sevilla hawajashindwa katika mechi 15 za ligi zilizopita huku wakipata sare 8 na kushinda mara 7.
Vile vile, Sevilla hawajashindwa katika mechi saba za ligi wakiwa ugenini huku wakiandikisha ushindi mara mbili mfululizo na sare tano mfululizo.
Mechi ya mwisho ya ligi baina ya Barcelona na Sevilla ilikuwa Disemba 21 2021.
Mechi hiyo iliishia kwa sare ya 1-1 ugani Estadio Ramón Sánchez ambao ni uwanja wa tatu kwa ukubwa Andalusia.
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi
Mechi - 5
Barcelona - 2
Sevilla - 0
Sare - 3
Ratiba ya La Liga, mechi ya 30
Jumamosi, Aprili 2
3:00pm- Getafe CF v Real Mallorca
5:15pm - UD Levante v Villarreal CF
7:30pm - Celta Vigo v Real Madrid
10:00pm Atletico Madrid v Deportivo Alaves
Jumapili, Aprili 3
3:00pm - Athetic Bilbao v Elche CF
5:15pm - Real Betis v CA Osasuna
7:30pm - Granada CF v Rayo Vallecano
7:30pm - Valencia CF v Cadiz CF
10:00pm - FC Barcelona v Sevilla FC
Jumatatu, Aprili 4
10:00pm- Real Sociedad v RCD Espanyol
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.