WAKATI YANGA WAKITAKA BIL 1...FEI TOTO AFUNGUKA HAKUNA WA KUMZUIA KWENDA SIMBA


Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo 


Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Azam, Feisal Salum 'Fei Toto' amesema kuwa kwa sasa hakuna mtu wa kumzuia kwenda klabu yoyote anayotaka kwenda.
 
Pamoja na vilabu vingine ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, Klabu ya Simba ni miongoni mwa timu zinazotajwa kuiwania saini ya nyota huyo mzaliwa wa Visiwa vya Zanzibar.
 
“Kwa sasa nina mkataba na Azam FC, lakini hakuna klabu inayozuiwa kwenda kwa uongozi wa klabu yangu kama inanihitaji na mimi nitakuwa tayari kama klabu zikikubaliana," amesema Fei Toto.
 
Itakumbukwa kuwa Yanga wameweka kipengele cha kulipwa Bilioni 1 endapo Azam watataka kumuuza Fei Toto kwenye timu yeyote ya Tanzania.
 
AZIDI KUMKIMBIZA AZIZ KI.
 
Timu ya Azam FC, Jana imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
 
Mabao ya mchezo huo yamefungwa na mshambuliaji Abdul Suleiman ‘Sopu’
dakika ya 30, huku Feisal Salum ‘Fei Toto’ akipiga msumari wa mwisho dakika ya 90.
 
Azam ambayo inagombea nafasi ya pili katika msimamo wa ligi imefikisha pointi 63 baada ya michezo 28, pointi tatu mbele ya Simba ambayo inacheza baadaye dhidi ya Geita Gold kwenye Uwanja wa Azam Complex.
 
Fei Toto amezidi kukinyemelea kiatu cha ufungaji bora baada ya kufunga bao la 16 na kumzidi Stephane Aziz KI wa Yanga mwenye 15.
 
Mchezo mwingine uliochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ulishuhudia Kagera Sugar ikikubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Coasta Union ambayo inaendelea kujiweka vizuri kwenye nafasi ya nne ya msimamo ikiwa na pointi 41 kwenye mechi 28, huku Kagera ikiendelea kusalia nafasi ya 10 ikiwa na pointi 31 kwenye mechi 28.
 
Mabao ya Coastal Union yamefungwa na Shedrack Mulingwe dakika ya 16 pamoja na Denis Modzaka aliyefunga la pili dakika ya 69, ilihali bao la kufutia machozi la Kagera limefungwa na Mbaraka Yusuphu dakika ya 73.
 

Sio Michezo wala Kasino, Betway hatupoi!

Anza safari yako ya kubashiri na Betway. Jisajili kwa Promo Code: SIMUJANJA24, cheza na Ushinde SAMSUNG S20 au S24 MPYAA! Kila wiki, tunatoa Mshindi wa Simu kwa wiki 8 mfululizo kuanzia Mei 6 hadi Juni 30.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway

 

Published: 06/03/2024