'MASHINE HII' IKITUA TU...YANGA MJIANDAE KUKABIDHI UBINGWA KWA SIMBA MSIMU UJAO...


Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo 


KATIKA Kuhakikisha wanaimarisha kikosi cha timu ya Simba msimu ujao, kikosi kazi maalum cha Wekundu wa Msimbazi hao, wamewasili nchini Zambia, kuzungumza na Winga wa Power Dynamos, Joshua Mutale.
 
Nyota huyo aliyecheza kwa kiwango cha juu kwenye mchezo wa ligi ya Mabingwa Afrika baina ya Simba na kupelekea kupatikana kwa goli la kwanza na mechi kuamuliwa kwa sare ya 2-2 nchini Zambia.
 
Winga huyo wa Zambia alionekana kumsumua beki wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe akiwa na jezi namba 7 mgongoni, kiwango alichokionyesha kimewashawishi mabosi wa Wekundu hao kuendelea na mawindo yao dhidi yake.
 
Imeeleza kuwa Simba imetuma watu wake nchini humo kwenda kuzungumza na kumaliza dili la kumpa nyota huyo na kumfanya kuwa sehemu ya usajili wa Wekundu wa Msimbazi kwa msimu ujao wa mashindano.
 
Taarifa zilizopatika kuwa usajili unafanyika kulingana na mapendekezo na mahitaji ya timu hiyo kulingana na nafasi zenye mapungufu na kuhakikisha wanaleta wachezaji watakaosaidia timu hiyo kutoka ilipo na kurejea katika makali yake.
 
“Kama alivyosema Mwenyekiti wa Bodi, Dewji (Mohammed) kuwa atafanya usajili mzuri kwa kuleta wachezaji wenye ubora, Mutale miongoni mwa wachezaji waliopo katika mipango yetu na kuna watu wameenda Zambia kwa ajili ya kufanya mazungumzo.
 
Tutafanya usajili mzuri na kuleta wachezaji watakaokata kiu ya mashabiki na na kuleta kocha mwenye hadhi ambaye ataiondoa Simba hapo ilipo na kurejesha soka letu la ‘Pira Biriani’ ambalo limepotea muda mrefu,”
amesema Mtoa habari huyo.
 
Meneja wa Idara ya habari na mwasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema suala la usajili linaenda vizuri na itakapofika muda sahihi wataweka wazi wamewasijili kina nani.
 
Amewataka wanasimba kuwa watulivu kipindi timu ipo mikononi mwa mwekezaji Mo Dewji kwa kuwapa ushirikiano viongozi kwa kupata utulivu wa kuisuka Simba mpya wanayoitaka.
 
“Baada ya kipindi kigumu cha mpito sasa tunajenga Simba mpya na imara kusajili wachezaji bora na kuleta matokeo mazuri, ukizingatia Tajiri ameanza kuingia sokoni akisaidiana na timu yake kuangalia aina ya wachezaji kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi,” amesema Ahmed.

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Bashiri popote

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Sio Michezo wala Kasino, Betway hatupoi!

Anza safari yako ya kubashiri na Betway. Jisajili kwa Promo Code: SIMUJANJA24, cheza na Ushinde SAMSUNG S20 au S24 MPYAA! Kila wiki, tunatoa Mshindi wa Simu kwa wiki 8 mfululizo kuanzia Mei 6 hadi Juni 30.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway

Published: 06/18/2024