Hakimiliki ya picha: Getty Images
2024 French Open
ITF
ATP Tour
WTA Tour
Stade Roland Garros
Paris, France
Mei 26 – Juni 9 2024
Shindano la tenisi la French Open 2024 linaendelea kule
Stade Roland Garros mjini Paris, Ufaransa baada ya kung’oa nanga Mei 26 na linatarajiwa kufikia kikomo mwezi Juni tarehe 9.
Kuhusu shindano hili.
Shindano hili linalojulikana kama Roland-Garros ni shindano kubwa la tenisi linaloandaliwa kwa kipindi cha zaidi ya wiki mbili Stade Roland Garros mjini Paris nchini Ufaransa kuanzia mwishoni mwa mwezi Mei kila mwaka.
Shindano la tenisi la French Open liliasisiwa mwaka 1891 na huchezewa kwenye sakafu ya udongo na ni shindano la pekee la Grand Slam kuchezewa katika sakafu ya udongo.
Habari za shindano hili
Stefanos Tsitsipas, Carlos Alcaraz, Grigor Dimitrov na Jannik Sinner ni wachezaji wanne waliofuzu hatua ya robo fainali kwa upande wa wanaume mchezaji mmoja kila upande Jumanne Juni 4.
Kwa upande wa wanawake, Iga Swiatek, Markéta Vondrousova, Coco Gauff na Ons Jabeur wamefuzu kuingia hatua ya robo fainali mchezaji mmoja kila upande Jumanne Juni 4.
Wanaopigiwa upatu
Mabingwa watetezi wa shindano hili mchezaji mmoja kila upande kwa wanaume Novak Djokovic na Swiatek kwa upande wa wanawake wanapigiwa upatu kutetea mataji yao katika shindano la mwaka huu la French Open.
Aryna Sabalenka anayeshikilia nafasi ya pili kwa wanawake duniani kwa mujibu wa shirikisho la tenisi duniani kwa wanawake(WTA) anatarajiwa kutoa ushindani mkali kwenye taji la mchezaji mmoja kila upande.
Kwengineko, Alexander Zverev aliye katika nafasi ya nne duniani kwa mujibu wa shirikisho la tenisi ,(ATP) anatarajiwa kutoa changamoto kubwa kwenye shindano la wanaume mchezaji mmoja kila upande.
Tuzo
Washindi wa shindano la French Open mwaka huu, mchezaji wa kiume na wa kike watapokea Euro milioni 2.4 kila mmoja huku washiriki wa fainali wakipata Euro milioni 1.2.
Bingwa wa kiume mchezaji mmoja kila upande atapata kombe liitwalo Coupe des Mousquetaires (The Musketeers' Cup) huku bingwa wa shindano la wanawake mchezaji mmoja kila upande akipata kombe liitwalo Coupe Suzanne Lenglen (Suzanne Lenglen Cup).
Nukuu
"Sio rahisi kucheza dhidi ya rafiki yangu. Nimemfahamu Hubi kwa miaka kadhaa sasa,” alisema Dimitrov baada ya kumshinda rafiki yake Hubert Hurkacz 7-6(5), 6-4, 7-6(3) kufuzu robo fainali.
"Tunafanya mazoezi pamoja. Tumeshiriki mambo kadhaa kwa pamoja na nilijua wazi kuwa mechi hii haitakuwa rahisi na nilihitaji juhudi za ziada. Nilitamani sana kufika wiki ya pili.
"Roland-Garros ni shindano la pekee la Grand Slam nililokuwa na wasiwasi kuwa singepata mafanikio makubwa lakini leo miaka 15 baadaye nimefuzu. Nina furaha kubwa kwa sababu hiyo.”
Washindi watano wa mwisho wa French Open mchezaji mmoja kila upande kwa wanaume.
2019 - Rafal Nadal (Uhispania)
2020 - Rafal Nadal (Uhispania)
2021 - Novak Djokovic (Serbia)
2022 - Rafal Nadal (Uhispania)
2023 - Novak Djokovic (Serbia)
Washindi watano wa mwisho wa French Open mchezaji mmoja kila upande kwa wanawake
2019 - Ashleigh Barty (Australia)
2020- Iga Swiatek (Poland)
2021 - Barbora Krejcíkova (Czech Republic)
2022 - Iga Swiatek (Poland)
2023 - Iga Swiatek (Poland)
Bashiri tenisi mtandaoni
Bashiri manguli kwenye michuano bora ya tenisi kutoka Wimbledon hadi Roland Garros. Jisajili leo na anza kubashiri kwenye machaguo tofauti ambayo tenisi inakupatia; kutoka 1x2 matokeo ya mechi, bashiri kwa mchezaji wako unayempenda hadi kwenye bashiri nyingi kama Mshindi wa Set. Chochote unachochagua kufanya, Betway ina chaguo kwaajili yako.
Sio Michezo wala Kasino, Betway hatupoi!
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway