Hakimiliki ya picha: Soka la Bongo
Mabosi wa
Simba SC wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’ wamefanikiwa kuinasa saini ya Kiungo Mshambuliaji kutoka Niger Victorien Adebayor muda mchache kabla ya kuivaa Taifa Stars juzi Jumapili (Juni 18).
Mabosi wa timu hiyo wamekuwa wakipambana kuhakikisha wanaijenga upya timu yao kufuatia kufanya vibaya misimu miwili mfululizo kwa kushindwa kutwaa mataji.
Katika Ligi Kuu Bara wamemaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Mabingwa Young Africans wakati kwenye Kombe Shirikisho ‘ASFC’ wakiishia Nusu Fainali huku Ligi ya Mabingwa Barani Afrika wakimaliza kwenye Robo Fainali.
Kufanya vibaya huko kumepelekea mabosi wa timu hiyo kuanza kushusha vyuma mapema ikiwa tayari wamekamilisha usajili wa mshambuliaji Onana Esomba kutoka Rayon Sport ya Rwanda kabla Jumapili (Juni 18) kukamilisha usajili wa Abebayor ambaye alikuwa nchini na timu yake ya Taifa ya Niger.
Vigogo wa Simba SC walichokifanya kuweza kufanya mazungumzo na mshambuliaji ya kukubali kujiunga na timu hiyo ni baada ya kuvamia kambi ya Niger iliyokuwa katikati ya mitaa ya Jiji la Dar ambapo ilifikia timu hiyo kabla ya kukubali kichapo cha bao 1-0 katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON’.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya timu hiyo zinaeleza kuwa Simba SC wamekubaliana kila kitu na winga huyo juu ya kujiunga na timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa kwa mkataba wa miaka miwili huku Simba SC wakilazimika kuwafuata RS Berkane ili kukamilisha usajili huo.
“Viongozi walimfuata mchezaji katika hoteli ambayo amefikia na timu yake na wamefanikiwa kufanya mazungumzo, mchezaji mwenyewe amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili lakini amewaeleza namna ambayo alikosa nafasi kubwa ya kucheza kule Morocco.
“Lakini kwa sasa kilichobakia ni kwa viongozi wa Simba kwenda RS Berkane kumaliza nao ili kila jambo likae sawa na kuna uwezo wa mtu kutumwa kwenda Morocco wakati wowote.”
Mtoa Taarifa huyo pia alisema kuwa, Adebayor atatambulisha hivi karibuni kwa ajili ya kuanza kuitumikia Simba kwenye mashindano mapya ya Caf Super League mwezi ujao.
Aidha pia inaelezwa kuwa mchezaji huyo atakuwa akilipwa mshahara wa Dola
9000 sawa na karibu Milioni 20 za kitanzania, huku akipewa posho na bonasi mbalimbali kulingana na kiwango chake.
Lakini kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Gain’, alishaweka wazi juu ya suala la kuboresha Benchi la Ufundi la timu hiyo kwa kusema kuwa wanayajua makosa waliofanya msimu huu hivyo wamejipanga kufanya maboresho makubwa katika eneo hilo ili kuweza kufanya vizuri msimu ujao.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.