UCL - Manchester City v Inter Milan


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 UEFA Champions League

Final

Manchester City v Inter Milan

Ataturk Olympic Stadium
Istanbul, Turkey
Saturday, 10 June 2023
Kick-off is at 21h00  
 
Manchester City watamenyana vikali na Inter Milan kwenye fainali ya kombe la klabu bingwa barani ulaya Ataturk Olympic Stadium mnamo Jumamosi Juni 10.
 
The Citizens walishinda taji la pili la ndani walipoibuka na ushindi wa 2-1 katika fainali ya kombe la FA dhidi ya majirani wao Manchester United Jumamosi iliyopita huku Ilkay Gundogan akifunga magoli mawili.
 
City chini ya Pep Guardiola walikuwa tayari wametetea taji la ligi baada ya kwenda michezo 12 bila kupoteza mechi hata moja na kuwapiku Arsenal ambao walikuwa wanaongoza ligi kwa alama 8 kufikia mwezi Aprili.  
 
City wanafukuzia taji lao la tatu msimu huu ili kuafikia mafanikio yaliyotimizwa na the Red Devils msimu 1998-99.

Henrikh Mkhitaryan
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Miamba hao wa soka England wanapigiwa upatu kuibuka kidedea kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo baada kupata ushindi wa 5-1 kwa ujumla dhidi ya Real Madrid katika hatua ya nusu fainali.
 
Hii ni mara ya pili timu hii kufika fainali ya shindano hili na wanatarajia kushinda safari hii kwani walipoteza fainali ya kwanza 1-0 dhidi ya Chelsea mjini Porto, Ureno misimu miwili iliyopita.
 
City hawajapoteza mchezo wa UEFA katika mechi 12 zilizopita msimu huu. Wameruhusu magoli matano tu na wamekosa kufunga goli katika mechi mbili tu huku zote zikitoka sare ya 0-0; dhidi ya FC Copenhagen na Borussia Dortmund katika hatua ya makundi.

Erling Haaland
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Erling Haaland amefunga magoli 12 katika mechi 10 msimu huu na ananuia kuingia katika orodha ya wachezaji waliofunga magoli 13 au zaidi katika msimu, mafanikio yaliyoafikiwa na Cristiano Ronaldo, Robert Lewandowski, Karim Benzema na Lionel Messi. Raia huyo wa Norway alikuwa na msimu wa kufana sana katika ligi ya Premier huku akifanikiwa kuvunja rekodi kadhaa na kufunga magoli 36 kwenye mechi 35.
 
Timu hizi zimekutana kwenye mechi za kirafiki tu huku Inter wakishinda mechi mbili 3-0 mwaka 2010 kabla ya City kushinda kwa magoli hayo walipokutana tena mwaka 2011.
 
Guardiola anasisitiza kuwa kikosi chake kinastahili pongezi kwa mafanikio ya misimu ya hivi karibuni huku akikiri kuwa ushindi wa ligi ya klabu bingwa ulaya utawapa heshima kubwa.  
 
"Imebaki mechi moja tu kuafikia mafanikio haya. Tunahisi tupo katika nafasi nadra ambayo pengine hatutaweza kufika tena,” alisema raia huyo wa Uhispania.
 
"Tutafanya mazoezi mara tatu au nne kujiandaa kwa ajili ya Inter Milan. Nina siku mbili kutazama na kuchambua mbinu zao kwani nilielekeza nguvu nyingi kuchambua United awali. Tutaingia kwenye mechi na lengo la kushinda kama ajuavyo kila mmoja.
 
"Tumekuwa na misimu ya kufana sana hivi karibuni. Tumeshinda ligi ya Premier, kombe la FA na Carabao. Limebaki kombe la UEFA. Litatupa heshima kubwa.
 
"Hata tusiposhinda kombe la UEFA, tayari tumekuwa na mafanikio makubwa kwa kweli. Ila tunatamani kulishinda. Ni jukumu letu na tuna nia ya kulishinda.
 
"Ni heshima kubwa. Umebaki mchezo mmoja tu. Ni fahari kubwa kwangu kufika fainali mbili na nusu fainali moja ya shindano hili katika kipindi cha misimu mitatu.
 
"Ni mafanikio makubwa tayari lakini tunahitaji kulishinda. Ni wazi kabisa. Pongezi sana kwa mafanikio yetu. Tumekuwa na mafanikio makubwa kwa misimu kadhaa.
 
"Niliwaambia wachezaji wangu kuwa wanahitaji kujituma zaidi ili kuweka kumbukumbu katika historia. Ni sharti washinde shindano la klabu ulaya.”
 

Takwimu baina ya timu hizi katika mashindano yote.

Mechi - 3
Man City - 1
Inter Milan - 2
Sare - 0
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 

Published: 06/09/2023