Serie A - SSC Napoli v US Sampdoria 


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 Italian Serie A

Matchday 38

SSC Napoli v US Sampdoria 

Stadio Diego Armando Maradona 
Naples, Italy 
Sunday, 4 June 2023 
Kick-off is at 15h00  
 
SSC Napoli watakuwa wenyeji wa UC Sampdoria katika mechi ya ligi ugani Stadio Diego Armando Maradona mnamo Juni 4.
 
Matokeo ya hivi karibuni
 
Napoli, maarufu kama the Little Donkey walitoka sare ya 2-2 na Bologna ugenini Mei 28 na hawajapoteza mechi ya ligi katika mechi mbili zilizopita.
 
Vile vile, Napoli hawajapoteza mechi ya ligi katika mechi nne zilizopita wakiwa nyumbani huku wakiandikisha sare mbili mfululizo na ushindi mara mbili mfululizo ugani Stadio Diego Armando Maradona.
 
Kwa upande mwingine, Sampdoria walilazimisha sare ya 2-2 dhidi ya US Sassuolo Mei 26 na kufikisha idadi ya mechi 10 za ligi bila ushindi.  
 
Vile vile, Sampdoria hawajashinda mechi yoyote ya ligi katika mechi 10 ugenini huku wakiandikisha sare mbili na kupoteza mechi nane.
 
Vikosi.
 
Hriving Lozano na Mario Rui ni wachezaji pekee wanaokosekana kwenye kikosi cha Napoli kutokana na majeraha.
 
Sampdoria hawana marufuku au adhabu ya mchezaji yeyote ila Ignacio Pussetto, Andrea Conti, Emil Audero, Gerard Yepes na Michaël Cuisance wanauguza majeraha.
 
Wachezaji muhimu
 
Mfungaji bora wa ligi ya Serie A na Napoli Victor Osimhen ambaye alifunga magoli mawili dhidi ya Bologna anatarajiwa kufunga tena hasa ukizingatia uzembe wa safu ya ulinzi ya Sampdoria.  
 
Manolo Gabbiadini ambaye alifunga goli lake la 11 la msimu dhidi ya Sassuolo atakuwa na shughuli nzito ya kuongoza timu yake kupata ushindi dhidi ya Napoli.

Manolo Gabbiadini
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Nukuu
 
“Mchezo unakuwa mgumu kwetu hasa wapinzani wanapomiliki mpira ukizingatia sifa za timu yangu,” meneja wa Napoli Luciano Spalletti alisema baada ya sare dhidi ya Bologna. 
 
"Tulihitajika kucheza vizuri zaidi japakuwa tulipata nafasi ya kushinda mchezo huo mapema. Bologna walijitahidi sana kusawazisha. Ni timu nzuri inayofundishwa vizuri.”
 
“Osimhen ni mchezaji mzuri mwenye nguvu na atafanikiwa katika timu yoyote atakayocheza. Ni mtu mzuri ambaye analeta suluhisho baina ya wachezaji wenzake,” aliongezea.
 
"Yeye huleta suluhisho katika changamoto. Ana mengi ya kujifunza na atazidi kuimarika kila uchao.”
 
Takwimu baina ya timu hizi
 
Napoli waliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Sampdoria kwenye mechi yao ya mwisho ya ligi iliyochezwa Januari 8 2023 ugani Stadio Comunale Luigi Ferraris.
 
The Little Donkeys hawajapoteza mechi ya ligi katika mechi nane za mwisho walizocheza dhidi ya Sampdoria huku wakiandikisha ushindi mara nane mfululizo.
 

Ratiba ya mechi za ligi kuu Italia mchezo wa 38


Juni 4 Jumapili.

Atalanta BC v AC Monza
 
US Cremonese v US Salernitana
Empoli FC v SS Lazio
SSC Napoli v UC Sampdoria
AS Roma v Spezia Calcio
US Lecce v Bologna FC
US Sassuolo v ACF Fiorentina
AC Milan v Hellas Verona
Torino FC v Inter Milan
Udinese Calcio v Juventus FC
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 06/01/2023