La Liga - Villarreal CF v Atletico Madrid


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 Spanish La Liga

Matchday 38

Villarreal CF v Atletico Madrid

Estadio de la Cerámica
Villarreal, Spain
Sunday, 4 June 2023 
Kick-off is at 18h30 
 
Villarreal CF na Atletico Madrid watamenyana vikali katika mechi ya ligi kuu Uhispania Juni 4 ugani Estadio de la Cerámica.
 
Matokeo ya hivi karibuni
 
The Yellow Submarine walipoteza mechi ya ligi iliyopita 2-1 wakiwa ugenini dhidi ya Rayo Vallecano Mei 28 na kufikisha kikomo msururu wa mechi sita za ligi bila kushindwa.
 
Hata hivyo, Villarreal hawajapoteza mechi hata moja katika michezo minne ya mwisho ya ligi wakiwa nyumbani huku wakiandikisha ushindi mara nne mfululizo ugani Estadio de la Cerámica.
 
Kwa upande mwingine, Atletico walipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Real Sociedad nyumbani mnamo Mei 28 na kufikisha idadi ya mechi tatu mfululizo bila kushindwa katika ligi.  
 
Hata hivyo, Atletico maarufu kama the Mattress Makers hawajashinda mechi ya ligi katika michezo miwili iliyopita wakiwa ugenini baada ya kuandikisha sare moja na kupoteza mechi moja.
 
Vikosi
 
Villarreal watakosa huduma za Francis Coquelin, Raul Albiol na José Luis Morales ambao wanauguza majeraha.
 
Atletico watakuwa bila wachezaji Thomas Lemar, Memphis Depay, Marcos Llorente, Jan Oblak na Reinildo ambao pia wanauguza majeraha.
 
Wachezaji muhimu
 
Giovani Lo Celso anategemewa sana na Villarreal kuwavusha na changamoto ya Atletico baada ya kufunga goli katika mechi yao dhidi ya Vallecano.  
 
Antoine Griezmann amekuwa mchezaji wa kutegemewa sana na Atletico msimu huu na atakuwa na majukumu ya kuhakikisha timu yake inapata ushindi dhidi ya Villarreal.

Antoine Griezmann
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Nukuu
 
“Lengo letu lilikuwa kupigania nafasi za kushiriki ligi ya klabu bingwa ulaya hadi mchezo wa mwisho. Mvua nyingi iliathiri uchezaji wetu,” alisema meneja wa Villarreal Quique Setien baada ya kushindwa na Vallecano.
 
"Tunazingatia sana kumiliki mpira katika mbinu zetu. Hali ya uwanja ilituathiri sana hasa kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili Rayo walionyesha ufanisi mkubwa na kutumia nafasi zao vizuri kwenye hali hiyo.
 
“Tumefanikiwa sana na tunathamini mafanikio hayo. Tayari tulikuwa tumefuzu kucheza ligi ya klabu ulaya zikiwa zimesalia mechi tatu msimu kukamilika. Tumemaliza msimu katika nafasi ya tano.”
 
Takwimu baina ta timu hizi
 
Villarreal waliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Atletico katika mchezo wa mwisho wa ligi baina yao Agosti 21 2022 ugani Cívitas Metropolitano.
 
The Yellow Submarine hawajapoteza mechi ya ligi katika michezo mitatu iliyopita dhidi ya the Mattress Makers baada ya kuandikisha ushindi mmoja na sare mbili.
 

Ratiba ya mechi za La liga mchezo wa 38.


Juni 4 Jumapili

6:30pm - Real Mallorca v Rayo Vallecano

6:30pm - Real Sociedad v Sevilla FC
6:30pm - Real Madrid v Athletic Bilbao
6:30pm - Villarreal CF v Atletico Madrid
6:30pm - CA Osasuna v Girona FC
9:00pm - Real Betis v Valencia CF
9:00pm - Celta Vigo FC Barcelona
9:00pm - Real Valladolid v Getafe CF
9:00pm - Elche CF v Cadiz CF
9:00pm - RCD Espanyol v UD Almeria
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 06/01/2023