Hakimiliki ya picha: Getty Images
2023 French Open
ATP Tour
Semi-finals
Stade Roland Garros
Paris, France
Friday, 9 June 2023
Mchezaji nambari moja wa tenisi duniani upande wa wanaume Carlos Alcaraz anapania kuingia fainali yake ya sita mwaka huu wa 2023 atakapokutana na Novak Djokovic kwenye nusu fainali ya shindano la
French Open Ijumaa Juni 9.
Raia huyo wa Uhispania tayari ameshinda mataji manne mwaka huu tangu kurejea uwanjani baada ya kupata jeraha lililomuweka nje ya shindano la Australian Open mwezi Januari.
Alcaraz amekuwa akionyesha mchezo mzuri na kupata matokeo mazuri kwenye mechi za uwanja wa udongo wa Paris huku akipoteza seti moja tu kuelekea mechi ya nusu fainali dhidi ya Djokovic. Alcaraz aliibuka na ushindi wa seti tatu; 7-6, 7-5, 7-6 katika nusu fainali ya Madrid Open dhidi ya Djokovic mwaka jana.
Alcaraz alipita mafanikio yake ya awali katika shindano la Roland Garros alipomuondoa mchezaji nambari tano duniani Stefanos Tsitsipas kwenye hatua ya robo fainali na kuibuka na ushindi wa 6-2, 6-1, 7-6.
Alcaraz aliingia nane bora Kwa mara ya kwanza yangu mwaka 2022 kabla ya kubanduliwa na Alexander Zverev katika seti nne ikiwa ni mwaka mmoja baada kuondolewa katika raundi ya tatu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 na mshindi wa shindano la US Open 2022 anapania kufika fainali ya pili ya Grand Slam katika maisha yake kwenye mchezo huu na kukutana na mmoja wa wachezaji bora katika historia ya tenisi.
“Tangu mwaka jana nimekuwa na uchu wa kucheza dhidi ya Novak,” alisema. “Sote tunacheza katika viwango vya juu. Natazamia kucheza mechi hiyo. Nitafurahia.
“Kwangu ni heshima kubwa kupata fursa ya kuandika historia na kucheza na mchezaji wa kiwango hicho. Utakuwa mchezo mzuri Kwa upande wangu.”
Washindi watano wa mwisho wa French Open.
2022 – Rafael Nadal (Uhispania)
2021 – Novak Djokovic (Serbia)
2020 – Rafael Nadal (Uhispania)
2019 – Rafael Nadal (Uhispania)
2018 – Rafael Nadal (Uhispania)
Bashiri tenisi mtandaoni
Bashiri manguli kwenye michuano bora ya tenisi kutoka Wimbledon hadi Roland Garros. Jisajili leo na anza kubashiri kwenye machaguo tofauti ambayo tenisi inakupatia; kutoka 1x2 matokeo ya mechi, bashiri kwa mchezaji wako unayempenda hadi kwenye bashiri nyingi kama Mshindi wa Set. Chochote unachochagua kufanya, Betway ina chaguo kwaajili yako.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway