Hakimiliki ya picha: Soka la Bongo
BAADA ya kufanikiwa kukamilisha usajili wa kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’, kuwa mali rasmi ya
Azam FC, ameahidi kufanya makubwa ndani ya kikosi cha timu yake hiyo mpya kwa msimu ujao wa mashindano.
Kiungo huyo tayari ametangazwa rasmi jana kuingia mkataba wa muda mrefu na Azam FC kwa kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mitatu hadi 2026.
Fei Toto alisema kile ambacho amekuwa akifanya ndani ya klabu yake ya zamani, anatarajia kukuonyesha akiwa na timu yake hiyo mpya kwa kufikia malengo yanayotarajiwa kwa msimu ujao.
Alisema anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa agizo lake kwa viongozi wa Yanga kumaliza mgogoro wao na hatimaye kufanikiwa kusaini mkataba kuitumikia Azam FC.
Baada ya kujiunga na Azam FC, kiungo huyo alitolea ufafanuzi kuhusu pesa alizochangisha kwenda CAS ambapo alisema pesa hizo ataenda kuzitoa kwenye shughuli za kijamii.
“Zile pesa siwezi kuzirejesha kwa walionitumia maana ni watu wengi na sitawajua wote, kwa hiyo nitazipeleka kwa watoto yatima, msikitini na makanisani kwa watu wanaouhitaji siwezi kuzitumia,” alisema Fei Toto.
Katika hatua nyingine uongozi wa Azam FC umeweka wazi kuwa wataendelea kuboresha kikosi cha timu yao kulingana na mahitaji ya benchi lao la ufundi linalonolewa na Kocha Youssouph Dabo.
Katika maboresho hayo ni kufanya usajili mzuri kulingana na mahitaji lakini pia kuhakikisha wanawazuia kwa kuwaongezea mikataba baadhi ya wachezaji wao muhimu ambao mikataba yao iko ukingoni.
Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin (Popat ) amesema wamedhamilia kuboresha kikosi chao na kuhakikisha wanafanya usajili wa wachezaji bora na kuwaongeza mikataba nyota wale wako kwenye mipango ya timu yao kwa msimi ujao.
Miongoni mwa wachezaji hao ni Bajana ambaye katika kipindi cha kuelekea usajili akihusishwa na klabu ya Simba ambao wanahitaji huduma ya nyota huyo.
Aidha katika hatua nyingine, Fei Toto amesema anarudi Zanzibar kwa wiki moja kwenda kufanya mazoezi na kupumzisha akili kutokana na kuwa na 'stress' za kukaa nje ya uwanja muda mrefu akifuatilia sakata lake.
"Naenda kufanya mazoezi alafu napumzika kwasababu nimekaa nje sana na lile sakata limeenda muda mrefu na stress zilikuwa nyingi kwahiyo nataka nikapumzishe akili ili nije kufanya kazi vizuri,"
Fei Toto amesema anaenda kukaa kwa wiki moja kisha atarudi kazini kuanza kujiandaa na msimu ujao.
Azam itacheza mechi ya mwisho ya Ligi Kuu kesho Juni 9 dhidi ya Polisi Tanzania ambayo tayari imeshashuka daraja katika Uwanja wa Azam Complex na Jumatatu itakuwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kucheza dhidi ya Yanga fainali ya Kombe la Shirikisho.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.