EPL - Wachezaji watano bora wa ligi ya Premier msimu wa 2022-23


Hakimiliki ya picha: Soka la Bongo


Msimu huu wa 2022-23 wa ligi ya Premier ulikuwa na panda shuka zake na hatimaye Manchester City wakatawazwa mabingwa.
 
Arsenal FC walipoteza nafasi ya kushinda taji hilo baada ya kuongoza ligi kwa muda mrefu huku nao Aston Villa na Brighton and Hove Albion wakicheza soka ya kuvutia na kuacha kumbukumbu nzuri msimu huu.
 
Chelsea FC na Liverpool FC walikuwa na msimu wa matokeo mseto na kumaliza nje ya nne bora huku nafasi hizo zikichukuliwa na Newcastle United na Manchester United.
 
Tuzame sasa na kuangazia wachezaji watano bora wa msimu 2022-23 wa ligi ya Premier.  
 
Bukayo Saka
 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alikuwa na mchango mkubwa katika juhudi za Arsenal msimu huu akifunga magoli 14 na kusaidia kupatikana kwa mengine 11.
 
Saka alishinda tuzo la mchezaji bora wa ligi wa mwezi Machi 2023 na pia kuteuliwa miongoni mwa wachezaji wa kushindania tuzo la mchezaji bora wa msimu.
 
Mchezaji huyo wa kimataifa wa England anakisiwa kuwa mmoja kati ya wachezaji bora wa pembezoni katika ligi ya Premier.
 
Marcus Rashford 
 
Msimu 2022-23 umekuwa msimu bora zaidi kwa mshambuliaji huyo wa Manchester United tangu alipojiunga na kikosi cha kwanza mwaka 2015.
 
Rashford alifunga magoli 17 katika ligi na kushinda tuzo la mchezaji bora wa mwezi mara nyingi zaidi kuliko mchezaji yeyote msimu huu.
 
Alishinda tuzo hilo mwezi Septemba 2022, Januari 2023 na Februari 2023.
 
Kevin De Bruyne 
 
Raia huyo wa Ubelgiji aliendelea kuonyesha weledi na uwezo wake mkubwa katika timu ya Manchester City na kuisaidia kutetea taji la ligi kwa mara ya tatu mfululizo.
 
De Bruyne alipika magoli mengi zaidi kuliko mchezaji yeyote baada ya kuchangia magoli 16 na vile vile kushinda tuzo la kiungo bora wa msimu kwa mara ya tatu.
 
Ushirikiano wa De Bruyne na mshambuliaji Erling Haaland ulichangia pakubwa katika mafanikio ya City.
 
Harry Kane 
 
Msimu huu wa 2022-23 tulishuhudia nyota huyo wa Tottenham Hotspur akivunja rekodi kadhaa huku pia akitajwa kuwa miongoni mwa washambuaji bora katika historia ya ligi hii.
 
Kane alimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Erling Haaland kwenye orodha ya wafungaji bora akiwa na magoli 30. Vile vile, ni mchezaji wa kwanza kufunga magoli 30 au zaidi katika misimu miwili tofauti ya mfumo mpya wa ligi.  
 
Mshambuliaji huyo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli 185 katika ligi ya Premier akiwa na timu moja na sasa ana magoli 213.
 
Erling Haaland 
 
Akitajwa na wengi kuwa mshambuliaji bora duniani, mchezaji huyo wa Manchester City alikuja kwenye ligi hii na kufanya ufungaji wa magoli kuonekana jambo la kawaida huku akizidi kuandikisha rekodi mpya.
 
Haaland alishinda kiatu cha dhahabu kwa kuibuka na magoli 36 katika michezo 35. Hii ni idadi kubwa ya magoli kufungwa ndani ya msimu katika historia ya ligi ya Premier.
 
Mchezaji huyo ambaye ni raia wa Norway alishinda tuzo mbili za mchezaji wa mwezi, mchezaji mchanga wa ligi wa msimu na pia mchezaji wa ligi wa msimu.  
 

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 
 

Published: 06/26/2023