Hakimiliki ya picha: Getty Images
Al Ahly imemuweka sokoni wing wake Jose Miquissone akiuzwa dola 250,000 (Sh 590 milion).
Katika kumweka sokoni, Simba ndio klabu iliyopewa kipaumbele cha kuulizwa kama itamhitaji kutokana na mkataba wake wakati anauzwa kuwa na kipengele.
Simba tayari imeshaanza mazungumzo na Luis ambaye amewataka mabosi wa Simba kufika kwenye mshahara wa Dola 20,000 (Sh 47 milion) kwa mwezi ili arejee nyumbani.
Dau ilo linaonekana kuwapasua vichwa mabosi wa Simba ambao walikuwa tayari kumpa mashahara wa Dola 10,000 (Sh 24milion).
Hata hivyo kwa uchunguzi wa Soka la Bongo, hakuna mchezaji anayelipwa zaidi ya dola 8 ndani ya simba huku ikitazamiwa rekodi hiyo huenda ikavunywa na Luis Miquissone kama mambo yataenda sawa.
Luis aliuzwa na Simba kwenda klabya Al Ahly ya nchini Misri kwa dau ambalo mabasi wa Msimbazi waligoma kuweka wazi japo duru za ndani zinadai kuwa aliuzwa kwa tahamani ya Bilioni 1.5.
Toka ajiunge na miamba hiyo ya kaskazini mwa afrika, Luis amekuwa hana nafasi ya kucheza mara kwa mara hali iliyopelekea kutolewa kwa mkopo mara moja nchini Saudi Arabia.
Wakati hali ikiwa hivyo kwake, Simba nako kwenyewe wamekuwa wakihaha kutafuta mbadala wake huku wachezaji wote waliowahi kusajiliwa na waliopo wakishindwa kuziba pengo la mshambuliaji huyo wa kimataifa kutoka Msumbiji.
Katika kutaka kuziba pengo lake, Simba kwa nyakati tofauti wamewasijili wachezaji kadhaa, huku wachezaji wa mwisho ambao bado wako ni pamoja na Pape Sakho, na Peter Banda, ambapo wote ni kama wameshindwa.
Luis aliouzwa pamoja na Clatous Chama , ambapo yeye alirudi kwenye dirisha dogo la usajili wa msimu wa 2021/22 na mpaka sasa bado yuko na wekundu hao wa msimbazi.
Simba SC wako kwenye mpango kazi wa kujijenga upya mara baada ya kutofanya vizuri katika misimu zaidi ya miwili mtawalia.
Katika misimu hiyo, Simba wameshuhudia wakipoteza makombe yote ya ndani kwa wapinzani wao wa jadi klabu ya Yanga SC huku pia wakishindwa kuwika kwenye mashindani ya kimataifa.
Duru za kiuchunguzi ndani ya klabu hiyo, iliyoletea Tanzania sifa kubwa kimataifa zinadai kuwa sababu ya mwekezaji na Rais wa heshima kwa klabu hiyo Ndg Mohammed Dewj kujiweka kando mwanzoni mwa msimu wa 2021/22 zimechangia kuidhoofisha klabu hiyo kubwa zaidi katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
Katika kipindi hiko, Simba ilishindwa kuwa na bajeti ya kutosha ya usajili pamoja na uendeshaji hali iliyopelekea kufanya usajili wa wachezaji wasiokizi matakwa na mahitaji ya soka la ushindani.
Wakati wao wakijivuta vuta na mambo hayo, wenzao Yanga waliiunuka na kufanya uwekezaji mkubwa kwenye kikosi chao hali iliyowafanya kuanza kuipa ushindani Simba na hatimaye kuivua ubingwa wa Ligi kuu na mataji mengine ya ndani.
Kwa takribani misimu minne nyuma, Simba walitawala soka la Tanzania kwa kubebea kila kombe ambalo walishiriki huku wakiwaacha wapinzani wao wakubwa Yanga kwenye hali ya huzuni.
Sasa Simba wamedhamiria kurudi kwa kishindo kikubwa , na ni suala la muda tu kuona kama kweli wako 'serious' au wanatania.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.