AFCON - Tanzania v Niger


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2023 Africa Cup of Nations Qualifiers

Group F

Tanzania v Niger

National Stadium
Dar es Salaam, Tanzania 
Sunday, 18 June 2023 
Kick-off is at 16h00 
 
Tanzania watakuwa mwenyeji wa Niger katika mechi ya kufuzu michuano ya kombe la mataifa barani Afrika (AFCON) 2023 mnamo Juni 18 mjini Dar es Salaam
 
Matokeo ya hivi karibuni
 
Timu ya taifa ya Tanzania ya wanaume maarufu kama Taifa Stars imeshinda mechi mbili kati ya mechi tatu za kundi F zilizopita na mataumaini ya kufuzu kucheza fainali hizi bado yapo hai baada ya kuandikisha ushindi mmoja, sare moja na kupoteza mechi mbili.
 
Hata hivyo, Tanzania hawajashinda mechi hata moja kati ya mechi mbili za mwisho za kufuzu AFCON wakiwa nyumbani huku wakipoteza mechi mbili mfululizo.  
 
Kwengineko, Niger hawajafanikiwa kushinda mechi hata moja kundi F ila bado wana nafasi ya kufuzu kushiriki AFCON baada ya kuandikisha sare mbili na kupoteza mechi mbili.
 
Niger, maarufu kama the Menas wamekuwa na matokeo mabaya ugenini baada ya kuandikisha sare mbili mfululizo na kupoteza mechi tatu katika mechi tano za mwisho wakiwa ugenini.
 
Wachezaji muhimu
 
Katika juhudi za kufuzu mashindano hayo, Tanzania wataweka matumaini yao kwa mshambuliaji mahiri na nahodha Mbwana Samatta ambaye amefunga magoli 22 katika mechi 71 za kimataifa.
 
Victorien Adebayor atakuwa mchezaji wa kutegemewa sana kwa upande wa Niger kwani amefunga magoli 19 katika mechi 53 za kimataifa.  
 
Nukuu
 
“Tulikuwa na fursa ya kupata ushindi,” kocha mkuu wa Tanzania Adel Amrouche alisema baada ya kushindwa na Uganda katika mechi ya kufuzu AFCON 2023 mnamo Machi 28.
 
"Hatukufanikiwa ila chochote kinawezekana. Tutajitathmini na kujiandaa vilivyo kwa mkondo wa mechi zinazofuata mwezi Juni. Naamini tutafanya vizuri.”
 
Takwimu baina ya timu hizi 
 
Timu hizi mbili zimekutana mara moja tu katika mashindano yote na mechi hiyo iliishia sare ya 1-1 mwezi Juni 2022.
 
Mechi hiyo ya kufuzu AFCON 2023 ilichezewa mjini Cotonou, Benin.
 

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 
 

Published: 06/14/2023