Verstappen apania ushindi wa kwanza British GP


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 FIA Formula One World Championship

2022 British Grand Prix

Silverstone Circuit
Silverstone, England
Sunday, 3 July 2022
 
Dereva wa Red Bull Racing Max Verstappen anapania kupata ushindi wa kwanza kabisa kwenye mbio za langa langa za British Grand Prix na kuendeleza msururu wa matokeo mazuri ya msimu 2022.
 
Raia huyo wa Uholanzi alichukua nafasi ya kwanza kwenye mbio za Canadian Grand Prix wiki mbili zilizopita ambao ulikuwa ushindi wake wa sita katika mbio tisa na nafasi ya jukwaani kwa mara ya saba mwaka huu.
 
Verstappen atakumbwa na upinzani mkali kutoka kwa Lewis Hamilton ambaye amekuwa na matokeo mazuri katika mkondo huo wa Silverstone Circuit hivi karibuni ikiwa ameshinda mbio hizo mara saba miaka minane iliyopita.

Lewis Hamilton
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Dereva huyo mwenye umri wa miaka 24 amemaliza katika nafasi ya pili mara mbili kwenye mbio hizo; 2016 na 2020 huku akilazimika kujiondoa kwenye mbio hizo baada ya mzunguko wa kwanza mwaka jana alipogongana na Hamilton.
 
Verstappen anaongoza jedwali la madereva kwa alama 46 mbele ya dereva mwenza wa Red Bull Racing Sergio Perez huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Charles Leclerc wa Ferrari.
 
Verstappen ambaye ni bingwa wa sasa wa dunia alimaliza sekunde  0.993 mbele ya Carlos Sainz katika mkondo wa Circuit Gilles Villeneuve na alikiri kuwa dereva huyo wa Ferrari alimpa ushindani mkubwa kwenye mbio hizo za Montreal.

Carlos Sainz Jr of FerrariHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
"Kwa ujumla zilikuwa mbio ngumu kwetu. Nilitarajia gari litakuwa na kasi zaidi lakini inaonekana Ferrari walijikaza sana,” alisema. “Tulilingana na Carlos. Haikuwa rahisi kushindana naye ukizingatia muda wa mzunguko.
 
"Sharti ujikaze. Makosa yoyote kwenye mizunguko kumi na tano ya mwisho yangekuwa na athari kubwa kwa sababu alikuwa karibu yangu muda wote.”
 

Matokeo ya mbio za Canadian Grand Prix 2022

 
Mshindi: Max Verstappen - Red Bull Racing
Nafasi ya pili: Carlos Sainz - Ferrari
Nafasi ya tatu: Lewis Hamilton - Mercedes
 

Bashiri Motosport na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 
 

Published: 06/30/2022