Ureno na Uhispania kukutana kwa mara ya 40


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 UEFA Nations League

League A - Group 2
Matchday 1

Spain v Portugal

Estadio Benito Villamarin
Sevilla, Spain
Thursday, 2 June 2022
Kick-off is at 21h45  
 
Uhispania wanatarajia kuendeleza ubabe wao dhidi ya Ureno watakapokutana kwenye mechi ya kwanza ya UEFA Nations League ugani Estadio Benito Villamarin Alhamisi Juni 2. 
 
La Furia Roja ya Uhispania imeshinda mara 18 katika mechi 39 walizocheza dhidi ya A Selecao ya Ureno, ambao wameshinda mechi sita tu japokuwa mechi nne za mwisho zimeishia kwa sare. 
 
Ureno ilikuwa mshindi wa kwanza wa shindano hili linaloandaliwa kila baada ya miaka miwili walipoishinda Uholanzi kwenye fainali ya 2018/19 huku Uhispania ikifika na kupoteza 2-1 katika fainali ya 2020/21 dhidi ya Ufaransa. 
 
Timu ya Luis Enrique imeshinda mechi nne mfululizo tangu walipopoteza dhidi ya Ufaransa kwa kushinda; 2-1 Albania na 5-0 dhidi ya Iceland kwenye mechi za kirafiki zilizocheza mwezi Machi mwaka huu.  

Luis Enrique
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Enrique alielezea mipango waliyonayo kuhusu mshambuliaji wa Barcelona Ansu Fati ambaye amekuwa akiuguza jeraha tangu alipoitwa kwenye kikosi cha taifa kwa mara ya kwanza. Mechi hiyo iliishia sare ya 1-1 dhidi ya Ujerumani na ilichezwa Septemba 3 2020. 
 
"Nina mipango maalum, hatutahatarisha,” alisema. “Tutamwangali kwa ukaribu kifanya mazoezi, hatacheza dakika nyingi. 
 
"Ni jambo kubwa kuitwa na kuwa kwenye mazingira ya timu ya taifa ambayo ni zawadi kubwa hata kuliko kushiriki mechi.” minutes."
 
Ureno inayofundishwa na Fernando Santos ililazimika kucheza mechi za mchujo ili kufuzu kombe la dunia 2022 nchini Qatar kwa kuwashinda Turkey 3-1 na North Macedonia 2-0 kwenye nusu fainali na fainali mtawalia. 
 
Serbia ilichukua uongozi wa kundi A kwenye mechi za kufuzu baada ya Ureno kushindwa katika mechi mbili za mwisho. 
 
Santos anatumai kuwa watakuwa na mchezo mzuri kwenye mechi za UEFA Nations League kama walivyocheza kwenye mechi za mchujo za kombe la dunia na kupata mafanikio kama ilivyokuwa miaka mitatu iliyopita.
 
"Ni sharti tuendeleze tulipoachia kwenye mechi za mchujo,” alisema. Tutacheza mechi nne za UEFA Nations League ndani ya siku kumi. Ni vizuri kuzingatia afya ya wachezaji kikamilifu. 
 
"Hili ni moja la shindano muhimu katika ratiba ya michezo na tunaenda kupambania ushindi.” 
 

Takwimu baina ya timu hizi

Mechi - 39
Uhispania - 18
Ureno - 6
Sare - 15


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 


 

Published: 06/01/2022