Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 UEFA Nations League
League A - Group 2
Matchday 3
Portugal v Czech Republic
Estadio Jose Alvalade
Lisbon, Portugal
Thursday, 9 June 2022
Kick-off is at 21h45
Ureno na the Czech Republic watapambania nafasi ya kwanza ya kundi 2 watakapokutana kwenye mechi ya
UEFA Nationas league Alhamisi Juni 9 Estadio Jose Alvalade.
The Selecao wanaongoza kundi hilo kwa wingi wa mabao zaidi ya Jamhuri ya Czech baada ya kuishinda Uswizi 4-0 Jumapili, hii ni baada ya kuanza kampeni hii kwa sare ya 1-1 dhidi ya Uhispania wiki iliyopita.
Vijana wa Fernando Santos wamepoteza mechi moja tu kati ya mechi 11 zilizopita na hawajapoteza mechi yoyote mwaka huu. Mwaka wa 2021 kwao uliisha kwa kupoteza 2-1 dhidi ya Serbia kwenye mechi ya kufuzu kombe la dunia.
Baada kushindwa na Serbia, Ureno ilihitaji kucheza mechi za mchujo ili kufuzu kombe la dunia na walishinda Turkey 3-1 nusu fainali kabla ya kuishindi North Macedonia 2-0 kwenye fainali.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Cristiano Ronaldo alifunga magoli mawili dhidi ya Uswizi na kufikisha 117 idadi ya magoli kimataifa, jambo lililomfurahisha mkufunzi Santos.
"Nahodha wangu ndiye bora duniani. Hakuna maneno zaidi ya kumwelezea tunaposema ndiye bora duniani. Nimeshasema jambo hili mara nyingi,” alisema.
"Mafanikio yake ni ishara tosha ya uwezo wake. Ni nahodha wa timu na anaonyesha mfano mzuri.”
Timu ya Czech ilianza kundi 2 kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Uswizi na walinusurika kiduchu kuishinda timu ya taifa ya Uhispania Jumapili.
Inigo Martinez wa Uhispania alifunga goli la kusawazisha dakika ya 90, bao lililopelekea mechi hiyo kuisha 2-2. Timu ya Czech ilitangulia kufunga dakika ya 4 (Jakub Pesek) na 65 (Jan Kuchta) kabla ya Uhispania kusawazisha. Mechi hiyo ilichezewa mjini Prague.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Jaroslav Silhavy alikiri kuwa timu yake ilizuia vizuri, hata hivyo anafuhia nafasi ya timu yake baada ya mechi mbili.
"Wachezaji wangu walijituma sana na mbinu zetu zilitufaidi japo tulizuia sana. Sidhani tulikuwa na jinsi nyingine ya kucheza mechi hii, na wachezaji wenyewe walielewa,” aliambia tovuti ya UEFA.
"Nitakiri kuwa, sikuamini tungekuwa na aIama nne baada ya mechi mbili hata kwenye ndoto. Tomas Soucek alisema kuwa hakufurahishwa na sare dhidi ya Uhispania. Hili linaonyesha malengo ya timu hii.”
Takwimu baina ya timu hizi
Mechi - 3
Ureno - 2
Jamhuri ya Czech – 1
Sare - 0
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.