Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 US Open
PGA Tour
European Tour
Japan Golf Tour
The Country Club
Brookline, Massachusetts, Boston, USA
16-19 June 2022
Shindano la gofu la
US Open 2022 litachezwa kuanzia tarehe 16 hadi 19 Juni Brookline, Massachusetts, Boston, Marekani. Haya yatakuwa makala ya 122 ya shindano hilo.
US Open ni shindano la tatu kati ya mashindano manne makubwa ya gofu, mengine yakiwa Masters, PGA Championship na British Open.
Shindano hili liliasisiwa mwaka 1985 na lipo kwenye ratiba rasmi ya PGA Tour, Japan Golf Tour na European Tour.
Hii itakuwa ni mara ya nne sehemu hiyo kuandaa shindano la US Open mara ya kwanza ikiwa; 1913, 1963, 1988.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Jon Rahm ndiye bingwa mtetezi wa US Open baada ya kushinda taji la mwaka 2021 na kulitoa kwa ajili ya mchezaji wa gofu raia wa Uhispania marehemu Seve Ballesteros.
Rahm atakuwa miongoni mwa wachezaji 156 watakaokuwa wakiwania dola milioni kumi na tano za shindano la mwaka huu. Wachezaji wanaoshikilia nafasi za kwanza 49 kwenye jedwali rasmi la gofu duniani wanapigiwa upatu kushinda shindano hili.
Raia huyo wa Uhispania na washindi wengine kumi wa US Open; Bryson DeChambeau (2020), Jim Furyk (2003), Dustin Johnson (2016), Martin Kaymer (2014), Brooks Koepka (2017, 2018), Rory McIlroy (2011), Justin Rose (2013), Webb Simpson (2012), Jordan Spieth (2015) na Gary Woodland (2019) hawatakiwi kushiriki mchujo ili kufuzu.
Mshindi mara sita wa Majors Phil Mickelson, mchezaji namba moja wa sasa duniani Scottie Scheffler na mchezaji aliyeshika nafasi ya pili ya US Open Louis Oosthuizen watashiriki shindano la mwaka huu, The Country Club.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
“Umoja wa mchezo wa gofu Marekani, USGA, inathamini wote walioonyesha nia ya kushiriki shindano la US Open,” alisema afisa mkuu wa USGA.
"Tumejitolea kuwapa fursa maelfu ya wacheza gofu nafasi ya kufuata ndoto yao ya kushiriki mashindano makubwa ya gofu.
“The U.S. Open ni shindano la kipekee kwa sababu katika ngazi ya kufuzu inatoa nafasi kwa wachezaji wa umri wote, rangi na uwezo,” aliongeza.
"Tunatazamia kuwakaribisha wachezaji 156 kwenye shindano ili kuonyesha uwezo wao The Country Club mwezi Juni.”
Willie Anderson, Bobby Jones, Ben Hogan na Jack Nicklaus wanashikilia rekodi ya walioshinda shindano hili mara nyingi huku wote wakishinda mara nne.
Washindi watano wa mwisho wa US Open
2017 - Brooks Koepka - Marekani
2018 - Brooks Koepka - Marekani
2019 - Gary Woodland - Marekani
2020 - Bryson DeChambeau - Marekani
2021 - Jon Rahm - Uhispania
Bashiri Gofu na Betway
Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.