Scheffler anapania ushindi, RBC Canadian Open


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 RBC Canadian Open 

US PGA Tour 

St. George's Golf and Country Club
Etobicoke, Ontario, Canada
9-12 June 2022 
 
Scottie Scheffler anapania kuendelea kusalia kileleni mwa jedwali rasmi la mchezo wa gofu kwa kushinda shindano la gofu la RBC Canadian Open 2022.
 
Mwendelezo wa mchezo mzuri wa raia huyo wa Marekani mapema mwaka huu ulipelekea yeye kuorodheshwa katika nafasi ya kwanza kwenye jedwali rasmi la gofu duniani.
 
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Scheffler kushiriki shindano la gofu la Canadian Open na ni mmoja kati ya wachezaji wanaopigiwa upatu kushinda shindano la mwaka huu.

Rory Mcllroy
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Mchezaji huyo mwenye talanta kubwa alishinda shindano la gofu la dunia la Dell Technologies Match 2022 kwa kumshinda Kevin Kisner miezi mitatu iliyopita.
 
Hivyo basi, Scheffler alikuwa mchezaji wa kiume wa 25 kushikilia nafasi ya kwanza duniani tangu bodi rasmi ya kusimamia gofu duniani ilipoasisiwa 1986.
 
Scheffler alimsinda Rory McIlroy kwenye shindano la gofu la Masters 2022 miezi miwili iliyopita na ulikuwa ushindi wake wa nne, mara sita alizoanza.
 
Kwenye mashindano makubwa yaliyofuata ya PGA Tour yaliyofanyika Aprili, mchezaji huyo chipukizi wa mwaka wa PGA Tour ya 2020 hakufanikiwa kufuzu kushiriki.

Kevin Kisner
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Katika mashindano yake rasmi ya mwisho ya Charles Schwab Challenge 2022, Scheffler alipoteza dhidi ya Sam Burns kwenye mechi ya raundi ya mchujo Mei 29.
 
Mshindi huyo wa shindano la gofu la WM Phoenix Open 2022 na Arnold Palmer Invitational 2022 anatazamia kwa ari kushiriki kwa mara ya kwanza shindano la Canadian Open.
 
“Ni heshima kubwa kushiriki shindano la kitaifa. Ni fahari kushiriki RBC Canadian Open mjini Toronto mwezi Juni kwa mara ya kwanza,” alisema Scheffler.
 
Leo Diegel ni mchezaji mwenye mafanikio makubwa katika historia ya mashindano ya gofu ya Canadian Open ikiwa ameshinda mara nne; 1924, 1925, 1928 na 1929.
 

Washindi watano wa mwisho wa Canadian Open

 
2015 - Jason Day - Australia 
2016 - Jhonattan Vegas - Venezuela 
2017 - Jhonattan Vegas -Venezuela 
2018 - Dustin Johnson – Marekani 
2019 - Rory McIlroy - Northern Ireland 
 

Bashiri Gofu na Betway

Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 
 

Published: 06/10/2022