Quartararo kutetea taji la mbio za Dutch MotoGP


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 MotoGP Season

2022 Dutch Grand Prix

Round 11
TT Circuit Assen
Assen, Netherlands 
Sunday, 26 June 2022

Fabio Quartararo ana imani ya kutetea kwa mafanikio taji la mbio za Dutch Grand Prix atakaposhiriki mbio hizo.
 
Mwendeshaji huyo wa Yamaha alikuwa na mafanikio katika mbio za Dutch MotoGP mwaka jana kwani aliibuka na ushindi kabla ya kushinda taji la dunia la mbio za MotoGP.
 
Quartararo yupo katika hali nzuri sasa hivi baada ya kushinda mbio za hivi karibuni ambazo zilikuwa German MotoGP mnamo Juni 19.

Johann Zarco of Ducati
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Quartararo mwenye umri wa miaka 23 aliongoza na kushikilia nafasi ya kwanza kwa mizunguko 30 na kushinda mbio za German MotoGP kwa takriban sekunde tano.
 
Waendeshaji wa Ducati Johann Zarco na Jack Miller walimaliza katika nafasi ya pili na tatu mtawalia huku kampuni hiyo ya Italia ikiwa na wikendi ya kufana.
 
Quartararo anaongoza jedwali la waendeshaji la 2022 huku akifuatiwa na Aleix Espargaro wa Aprilia na nafasi ya tatu kushikiliwa na Zarco.
 
Raia huyo wa Ufaransa ambaye anatarajia kushinda taji lake la pili la dunia la MotoGP mtawalia anataka kupanua uongozi wake kwa kushinda mbio za Dutch MotoGP. 
 
Franco Morbidelli of Yamaha
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
“Ukweli najihisi vizuri kila ninapokuwa kwenye mbio,” Quartararo alijibu alipoulizwa hisia zake baada ya kushinda German MotoGP. 
 
“Kila siku na kila mbio ni nafasi nyingine ya kujifunza. Haikuwa rahisi kushikilia nafasi ya kwanza kwa mizunguko 30 hapa.
 
“Mazingira ya Barcelona yalinisaidia sana kwa sababu nilikuwa katika hali kama hii lakini nahisi kuwa naendesha vizuri kuliko awali,” aliendelea.
 
“Najihisi furaha sana. Ni ushindi wa kipekee. Ilikuwa kama Barcelona.”
 
Ducati inashikilia nafasi ya kwanza kwenye jedwali la waundaji wakifutiwa na Yamaha kisha nafasi ya tatu inashikiliwa na Aprilia.
 

Matokeo ya mbio za Dutch MotoGP 2021

 
Mshindi: Fabio Quartararo - Yamaha 
Nafasi ya pili: Maverick Vinales - Yamaha
Nafasi ya tatu: Joan Mir - Suzuki 
 

Bashiri Motosport na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 

Published: 06/22/2022