Quarataro anatazamia ushindi mwingine, German MotoGP


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 MotoGP Season

2022 German Grand Prix

Round 10
Sachsenring
Hohenstein-Ernstthal, Germany 
Sunday, 19 June 2022

Fabio Quartararo anatazamia kuendeleza msururu wake wa matokeo mazuri atakaposhiriki mbio za pikipiki za German Grand Prix mnamo Juni 19. 
 
Mwendeshaji huyo wa Yamaha alimaliza kwenye nafasi ya tatu katika mbio za German MotoGP mwaka jana kabla ya kushinda taji la dunia la MotoGP 2021.
 
Quartararo ana imani atafanya vizuri kwenye mbio zinazofuata hasa baada ya kushinda mbio za hivi maajuzi za Catalan MotoGP Juni 5.

Jorge Martin
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Raia huyo wa Ufaransa alikuwa na mbio nzuri tangu mwanzo hadi mwisho kule Catalan na kuandikisha ushindi wake wa pili msimu, wa kwanza ukija kwenye mbio za Portuguese MotoGP Aprili 24. 
 
Jorge Martin na Johann Zarco wa Ducati ya Italia walimaliza katika nafasi ya pili na tatu mtawalia kwenye mbio hizo za nchini Uhispania.
 
Quartararo anasalia kileleni mwa jedwali la waendeshaji mwaka 2022 huku akifuatiwa na Espargaro na Enea Bastianini wa Ducati katika nafasi ya pili na tatu mtawalia.
 
Quartararo ambaye ni bingwa mtetezi anatarajia kupanua uongozi wake kwa kushinda mbio za German MotoGP ambazo hajawai kushinda.

Darryn Binder
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
“Nimefurahishwa sana, zilikuwa mbio za kufana. Nilianza vizuri na kumaliza vizuri,” alisema Quartararo baada ya mbio za Catalan MotoGP. 
 
"Ushindi huu na nafasi ya pili niliyopata Mugello Jumapili iliyopita ni matokeo mazuri sana kwani sikujua cha kutarajia kabla.
 
"Mambo yanaenda vizuri. Tumejituma zaidi. Nilijihisi vizuri tangu mwanzo na nilijua nataka ushindi huu sehemu za kwanza za mbio. Zilikuwa mbio nzuri. Nilijihisi vizuri,” aliongeza.
 
"Nilipambana sana tangu mwanzo na kila wakati nilikuwa nikiangalia gurudumu langu la nyuma na halikuwa na shida yoyote. Nina furaha sana.”
 
Ducati wanashikilia nafasi ya kwanza kwenye jedwali la kampuni, nafasi ya pili inashikiliwa na Yamaha huku nafasi ya tatu ikitwaliwa na Aprilia.
 

Matokeo ya mbio za German MotoGP 2021

 
Mshindi: Marc Marquez - Honda 
Nafasi ya pili: Miguel Olivieira - KTM
Nafasi ya tatu: Fabio Quartararo - Yamaha 
 

Bashiri Motosport na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 

Published: 06/14/2022