Nigeria kupambana na Sierra Leone


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2023 Africa Cup of Nations (AFCON) Qualifiers 

Group A

Nigeria v Sierra Leone 

Abuja National Stadium 
Abuja, Nigeria 
Thursday, 9 June 2022 
Kick-off is at 19h00  
 
Nigeria watakuwa mwenyeji wa Sierra Leone kwenye mechi ya kufuzu kombe la mataifa barani Afrika 2023 katika uwanja wa kitaifa wa Abuja Juni 9. 
 
The Super Eagles wakiwa nyumbani walipata sare ya 1-1 dhidi ya Ghana kwenye mechi ya mwisho ambayo ilikuwa ya kufuzu kombe la dunia 2022 mnamo Machi 29. 
 
Nigeria hawajashinda mechi yoyote kati ya tatu zilizopita huku wakiandikisha sare mbili mfululizo na kupoteza dhidi ya Tunisia.

Jose Peseiro
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Nigeria, ambao ni mabingwa mara tatu wa AFCON hawajashindwa katika mechi tano za mwisho za kufuzu AFCON wakiwa nyumbani. Hii ni baada ya kupata ushindi mara nne na sare kwenye mechi moja.
 
“Nadhani tulicheza vizuri zaidi dhidi ya Equador kuliko tulivyocheza dhidi ya Mexico,” alisema kocha wa Nigeria Jose Peseiro baada ya kupoteza 1-0 dhidi ya Equador katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Juni 3. 
 
“Tutacheza vizuri zaidi kwenye mechi inayofuata kuliko tulivyocheza mechi hii. Natumai tutafunga magoli tuliyokosa kwenye mechi hii ya leo katika mechi rasmi dhidi ya Sierra Leone. 
 
“Raia wa Nigeria wanafaa kuwa na furaha na timu ya Super Eagles kwa sababu ina wachezaji wazuri. Tuna wachezaji wengi walio na talanta tunachohitaji ni kuimarisha mipango, mifumo na kuwa na muendelezo.” 
 
Kwingineko, Sierra Leone walipoteza 1-0 dhidi ya Equatorial Guinea katika mechi yao ya mwisho ambayo ilikuwa ya AFCON 2021 na ilichezwa Januari 20.  
 
Sierra Leone hawajashinda mechi yoyote katika mechi tatu za mwsiho rasmi walizocheza huku waiandikisha sare mbili mfululizo na kushindwa mara moja. 
 
Hata hivyo, Sierra Leone hawajashinda mechi yoyote ya kufuzu AFCON kati ya mechi kumi na saba wakiwa ugenini baada ya kuandikisha sare saba na kushindwa katika mechi kumi.  
 
Mechi ya mwisho baina ya Nigeria na Sierra Leone ilikuwa mnamo Novemba 17 2020. 
 
Mechi hiyo ya kufuzu kombe la mataifa bara Afrika 2021 iliishia sare ya 0-0 na ulichezwa katika uga wa kitaifa wa Siaka Stevens, Freetown. 
 

Takwimu baina ya timu hizi katika mashindano yote

Mechi - 16
Nigeria - 9 
Sierra Leone - 2
Sare - 5


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 06/07/2022