Msumbiji yalenga kisasi dhidi ya Rwanda


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2023 Africa Cup of Nations (AFCON) Qualifiers 

Group L

Mozambique v Rwanda 

FNB Stadium 
Johannesburg, South Africa 
Thursday, 2 June 2022 
Kick-off is at 19h00  
 
Mozambique na Rwanda watamenyana katika mechi ya kufuzu kombe la mataifa Afrika 2023 ugani FNB Juni 2. 
 
The Mambas wakiwa nyumbani walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Malawi katika mechi yao ya mwisho ambayo ilikuwa ya kufuzu kombe la dunia 2022. Mechi ilichezwa mnamo Novemba 16 2021. 
 
Kabla ya mechi hiyo, msumbiji walikuwa wamecheza mechi tano wakiandikisha sare moja na kushindwa mechi nne.
 
Taifa hilo la Afrika ya kusini halijashinda mechi yoyote katika mechi mbili za mwisho za kufuzu kombe la mataifa Afrika wakiwa nyumbani kwani wamepoteza mechi zote mbili mfululizo. 
 
Kwingineko, Rwanda walipoteza 2-1 dhidi ya Kenya kwenye mechi yao ya mwisho ambayo ilikuwa ya kufuzu kombe la dunia 2022 na ilichezwa Novemba 15 2021. 
 
Katika mechi sita za mwisho, Amavumbi wamepoteza mechi tano na kupata sare moja. 
 
Vile vile, Rwanda haijashinda mechi yoyote ya ugenini kati ya mechi nane walizocheza wakati wa kufuzu kombe la AFCON baada ya kuandikisha sare tatu na kushindwa mechi tano. 
  
Carlos Alos Ferrer ambaye ni kocha mkuu wa Rwanda amesema kuwa wachezaji wake wapo katika hali nzuri kuelekea mechi dhidi ya Msumbiji. 
 
"Nimefurahishwa na wachezaji nilio nao. Wanajituma asilimia mia moja mazoezini. Kujitolea kwao kunanipa motisha ndani na nje ya uwanja. Tunajivunia kikosi hiki,” Alos aliambia jarida la New Times. 
 
"Jukumu langu ni kuwaandaa wachezaji kwa ajili ya mechi na kazi yao ni kutekeleza mbinu hizo uwanjani,” aliongeza. “Tutajituma kadri ya uwezo wetu.” 
 
Msumbiji na Rwanda walikutana mara ya mwisho katika mechi mnamo was onMachi 24 2021. 
 
Amavumbi, kama inavyofahamika timu ya Rwanda, walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya The Mambas ya Msumbiji kwenye mechi ya kufuzu AFCON 2021 iliyochezewa Stade Régional de Nyamirambo nchini Rwanda. 
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi zote. 

Mechi - 4
Msumbiji - 2
Rwanda - 2
Sare - 0
 

Ratiba ya mechi za kufuzu kombe la mataifa Afrika 2023

 
Alhamisi, Junei 2
 
Majira ya Afrika ya kati.
 
5:00pm - Malawi v Ethiopia 
 
7:00pm- Msumbiji v Rwanda 
 
10:00pm- Misri v Guinea 
 
10:00pm- Tunisia v Equatorial Guinea 


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 06/01/2022