Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 Travelers Championship
US PGA Tour
TPC River Highlands
Cromwell, Connecticut, USA
23-26 June 2022
Rory McIlroy anatazamia kushinda shindano la gofu la
Travelers Championship kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya mchezo wa gofu.
Raia huyo wa Northern Ireland ni miongoni mwa wachezaji wanaopigiwa upatu kushinda shindano hilo ikiwa tayari ameshinda mashindano mawili ya PGA Tour ya msimu huu wa 2021-22.
McIlroy ambaye anashikilia nafasi ya pili katika jedwali rasmi la gofu duniani alishinda shindano la gofu la CJ Open mwezi Oktoba mwaka jana kabla ya kunyanyua taji la RBC Canadian Open mnamo Juni 12.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kwa kushinda kombe la gofu la CJ, mwanagofu huyo mara tatu wa mwaka wa European Tour aliweka historia ya kuwa mchezaji wa sita kupata ushindi mara 20 kwenye PGA Tour kabla ya kufikisha miaka 33 tangu mwaka 1960.
McIlroy alikuwa nyuma mwanzoni mwa mizunguko miwili ya mwisho lakini ushindi wa 62-66 siku mbili za mwisho ulimpa ushindi dhidi ya Collin Morikawa.
Mchezaji huyo mwenye makao yake Florida alitetea taji lake katika shindano la RBC Canadian Open kwa mafanikio alipomshinda Tony Finau zaidi ya wiki moja iliyopita.
Jina lake la utani likiwa Rors, McIlroy anakuja katika shindano hili la gofu la Travellers Championship baada ya kumaliza wa tano katika shindano la hivi majuzi la US Open ambalo alishinda mwaka 2011.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
“Siku hii nitaikumbuka kwa muda mrefu,” alisema McIlroy baada ya kushinda shindano la 2022 la RBC Canadian Open.
“Nimeshinda PGA Tour mara 21. Mara moja zaidi ya kila mtu. Nilipata motisha kutoka kwa mpinzani wangu.
"Mchezaji anayeshiriki shindano hilo ameshinda mara 20 kwenye PGA Tour kama mimi. Nilikuwa nataka kushinda mara moja zaidi yake na nikafanikiwa. Nilifurahi sana n ani fahari kubwa.”
Billy Casper ndiye mchezaji aliye na mafanikio makubwa katika historia ya shindano la Travelers Championship ikiwa ameshinda mara nne; 1963, 1965, 1968 na 1973.
Mabingwa watano wa mwisho wa shindano la gofu Travelers Championship
2017 - Jordan Spieth - Marekani
2018 - Bubba Watson - Marekani
2019 - Chez Reavie - Marekani
2020 - Dustin Johnson - Marekani
2021 - Harris English - Marekani
Bashiri Gofu na Betway
Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.