Mbio za pikipiki, 2022 Catalan MotoGP kung’oa nanga


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 MotoGP Season

2022 Catalan Grand Prix

Round 9
Circuit de Barcelona-Catalunya
Montmeló, Spain 
Sunday, 5 June 2022
 
mbio za 2022 Catalan Grand Prix za pikipiki zitang’oa nanga Montmelo iliyopo manispaa Barcelona eneo la Catalonia nchini Uhispania Juni 5.
 
Huu utakuwa mzunguko wa tisa wa shindano la mwaka huu na utafanyika kwenye mkondo Circuit de Barcelona-Catalunya. 
 
Mwendeshaji pikipiki mstaafu Valentino Rossi ndiye mwenye mafanikio makubwa katika historia ya mbio hizi akiwa ameshinda mara sita. 
 
Mbio za hivi majuzi za 2022 MotoGP zilikuwa Italian Grand Prix zilizofanyika kwenye mkondo wa Autodromo Internazionale del Mugello mnamo Mei 29. 

Aleix EspargaroHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Francesco Bagnaia wa Ducati alishinda mbio hizo za Italian Grand Prix 2022 ambao ulikuwa ni ushinda wake wa pili wa msimu huu. 
 
Fabio Quartararo wa Yamaha alimaliza wa pili nchini Italia huku nafasi ya tatu ikitwaliwa na mwendeshaji wa Aprilia Aleix Espargaro kwenye mbio hizi za nane za msimu huu. 
 
Quartararo anasalia kileleni mwa jedwali la 2022 la waendeshaji akiwa na alama 122 kuelekea mbio za Catalan MotoGP. 
 
Espargaro na Enea Bastianini wa Ducati wanashikilia nafasi ya pili na tatu kwa alama 114 na 94 mtawalia wakipambana kumfikia Quartararo. 

Enea Bastianini
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Johann Zarco aliye nafasi ya tano kwenye jedwali la waendeshaji akiwa na alama 75 na alama sita nyuma ya Bagnaia wa nne, alifurahia kumaliza katika nafasi ya nne mbio za Italian MotoGP.
 
“Mizunguko ya kwanza haikuwa rahisi. Kila mmoja anakuwa na nafasi ya kupenya lakini sio wote wenye weledi katika mazingira hayo,” alisema Zarco.
 
"Nilifurahishwa na kasi ya mbio ambayo iliniwezesha kuungana na kikundi kilichokuwa kikiongoza. Aleix wa Espargaro na Fabio wa Quartararo waliongeza kasi na ndipo nikamzuia Marco wa Bezzecchi nyuma yangu. 
 
"Nilitumia nguvu nyingi sana hadi kwenye mzunguko wa wa mwisho. Nafasi ya nne sio mbaya.”
 
Ducati wanaongoza kwenye jedwali la waundaji, wakifuatiwa na Yamaha na Aprilia mtawalia. 
 

Matokeo ya mbio za pikipiki za Catalan Grand Prix 2021

 
Msindi: Miguel Olivieira - KTM
Nafasi ya pili: Johann Zarco - Ducati
Third-Place: Jack Miller - Ducati
 

Bashiri Motosport na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 06/02/2022