Hamilton atazamia taji la pili Azerbaijan GP


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 FIA Formula One World Championship 

Eight Round

2022 Azerbaijan Grand Prix

Azerbaijan Baku City Circuit
Baku, Azerbaijan 
Sunday, 12 June 2022
 
Lewis Hamilton anatarajia kuweka historia ya kuwa dereva wa kwanza kushinda mbio za langa langa za Azerbaijan Grand Prix mara mbili.
 
Dereva huyo wa Mercedes hakuwa na mbio nzuri za Azerbaijan Grand Prix baada ya kumaliza wa 15 na kukosa alama zozote.   
 
Changamoto za Hamilton za msimu huu ziliendelea kwenye mbio za hivi maajuzi za Monaco Grand Prix 2022 alipomaliza katika nafasi ya 8, Mei 29.

Charles Leclerc
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Dereva huyo Muingereza alitarajia kutakuwa na mvua kabla ya mbio hizo lakini alishindwa kuitumia fursa hiyo na muda mwingi alikuwa nyuma ya madereva wengine katika sehemu tofauti za mbio hizo na kumaliza kwenye nafasi ya nane.
 
Sergio Perez wa Red Bull Racing-RBPT alishinda mbio za Monaco Grand Prix huku dereva wa Ferrari Carlos Sainz Jr na Max Verstappen wa Red Bull wakimaliza katika nafasi ya pili na tatu mtawalia.
 
Verstappen anaongoza jedwali la madereva la 2022 akifuatiwa na Charles Leclerc kisha Sergio Perez anachukua nafasi ya tatu.
 
Hamilton ambaye ni bingwa mara saba wa dunia wa Formula One yupo katika nafasi ya nane kwenye jedwali na anatazamia kushinda mbio za Azerbaijan Grand Prix kwa mara ya pili. Hii ni baada ya kushinda mbio hizo mwaka 2018.

George Russell
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
“Nilikuwa na uwezo wa kutumia fursa hiyo, pengine. Sijaangalia ambacho kingewezekana kweli,” alisema Hamilton baada ya kushindwa kutumia mazingira ya mvua Monaco.
 
"Ni kibarua kigumu kuwa nyuma ya madereva hao wawili. Hata hivyo sikushangaa kwa sababu unaweza kutarajia hilo hapa Monaco.
 
"Nilifahamu kuwa, kuwa nyuma ya mmoja wao matokeo yangekuwa kama yalivyokuwa. Nilidhani mvua itanipa fursa wikendi hii lakini haikuwa hivyo.”
 
Kampuni ya Red Bull Racing-RBPT inaongoza jedwali la waundaji, nafasi ya pili inashikwa na Ferrari kisha nafasi ya tatu inatwaliwa na Mercedes.  
 

Matokeo ya mbio za Azerbaijan Grand Prix 2021 

Mshindi: Sergio Perez - Red Bull Racing-Honda 
Nafasi ya pili: Sebastian Vettel - Aston Martin-Mercedes 
Nafasi ya tatu: Pierre Gasley - AlphaTauri-Honda
 

Bashiri Motosport na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 

Published: 06/08/2022