Michezo ya Olimpiki 2024 - Mazoezi ya viungo


Hakimiliki ya picha: Alamy


Michezo ya Olimpiki 2024.
Mazoezi ya viungo
Bercy Arena (artistic and trampoline)
Porte de La Chapelle Arena (rhythmic)
Paris, Ufaransa
Julai 27 – Agosti 5 2024 (artistic)
8–10 Agosti 2024 (rhythmic)
Agosti 2 2024 (trampoline)
 
Mchezo wa mazoezi ya viungo umekuwa mmoja wa michezo ya Olimpiki tangu mashindano hayo kuasisiwa mwaka 1896. Mchezo huo unaohusisha kategoria tatu mwaka huu unatarajiwa kutoa ushindani mkali mashindano hayo yatakapong’oa nanga Jumamosi Julai 27.
 
Mchakato wa kufuzu umefanyiwa marekebisho na kurahisishwa ili kuwapa wachezaji nafasi nyingi katika kategoria tofauti ukilinganisha na mashindano ya 2020 mjini Tokyo.
 
China ilishika nafasi ya kwanza kwa wingi wa medali mwaka 2020 huku wakiwa na jumla ya medali 11 (dhahabu 4, fedha 5 na shaba 2). Nafasi ya pili ilikuwa Urusi wakiwa na jumla ya medali 10 (dhahabu 2, fedha 4 na shaba 4) huku nafasi ya tatu ikitwaliwa na Marekani wakiwa jumla ya medali 6, (dhahabu 2, fedha 2 na shaba 2).
 
Liu Yang, Zou Jingyuan, Guan Chenchen na Zhu Xueying walionyesha uwezo mkubwa kwa upande wa wanawake huku wakiibuka na matokeo ya kuvutia sana.
 
China (69) wanashikilia nafasi ya nne kwa ujumla wa medali lakini nafasi hiyo inatarajiwa kuimarika kwani wanatarajia medali zaidi kutoka kwa washiriki 20 wa michezo ya mazoezi ya viungo olimpiki ya mwaka huu. Ushindi wa medali zaidi kwa China utawapeleka karibu na Japan(103) walio katika nafasi ya tatu.
 
Guan Chenchen ni mshindi wa pekee wa medali ya dhahabu kati ya washindi wanne wa michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020 anayekosekana mashindano ya mwaka huu baada ya kustaafu mwezi Oktoba 2022 kuzingatia masomo yake.
 
Suggested photo: Zhu Xueying of China
 
Baada ya ushindi wa dhahabu mjini Tokyo, Zhu aliongeza dhahabu nyingine kwenye michezo yake ya kwanza ya bara Asia mjini Hangzhou mwaka uliopita na vile vile kupata ushindi kwenye mashindano ya kombe la dunia Varna na Baku mapema mwaka huu.  Matarajio yake ni kuwa juhudi zote hizi zitamsaidia kufanya vizuri mjini Paris. 
 
"Wazazi wangu wana hofu kuwa wanaweza kuathiri matokeo yangu. Hawapendelei kujadili na mimi kuhusu chochote nyumbani,” alisema.
 
"Japokuwa nina mafanikio mengi, sitilii maanani mafanikio hayo ninapokuwa kwenye shindano jipya kwani naamini kuna nafasi zaidi ya kuimarika.” 
 
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Bashiri popote

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 07/27/2024