KUHUSU ISHU YA LAMEK LAWI NA SIMBA...MAGORI AVUNJA UKIMYA...ATAJA PALIPOTIBUKA


Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo 


LICHA ya kutambulisha nyota 10 wapya, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Crescentius Magori ameweka wazi kubwa bado wanaendelea kushusha vifaa vingine vipya kwa ajili ya kutengeneza timu imara.
 
Amesema usajili haujakalimika wanaendelea kuongeza watu kulingana na mahitaji ya timu yao na huku kuendelea kupunguza wachezaji kupisha wapya kuingia.
 
Baadhi ya wachezaji ambao Simba imemsajili Lameck Lawi, Abdulrazack Hamza, Debora Fernandes, Augustine Okejepha, Ahoua Jean Charles, Steven Mukwala, Joshua Mutale na Valentino Mashaka.
 
Kwa mujibu wa Mjumbe huyo amesema wanahitaji kutengeneza timu mpya na kusajili wachezaji kulingana na vigezo ikiwemo umri wa wachezaji ambao watakuwa katika mipango yao ya muda mrefu.
 
“Tulihitaji kuwa na timu mpya, tukafanya mabadiliko makubwa, ukichelewa kubadilisha timu muda mrefu lazima yatokee haya yaliyotokea msimu uliopita
 
Tunaangalia mchezaji sio kwa mechi moja tulitulia na kujiridhisha juu ya usajili wetu, kuna mambo makubwa yanakuja.tumetumia wataalamu kufanya mabadiliko ya timu tunaamini vijana wenye vipaji na muda mfupi wanaweza kupeperusha bendera ya Taifa,” amesema Magori.
 
Kuhusu vijana wanaosajiliwa kushindwa kuingia  katika mfumo, amesema Simba na Yanga zinapresha kubwa, usipopata kocha hodari wa kuwapa nafasi wachezaji wageni na vijana katika kikosi cha kwanza, yanatokea kila baada ya miezi sita unamtoa kwa mkopo.
 
“Misimu mitatu Simba haijakosea kwenye usajili bali hatukuweza kushinda, kuna mambo matatu yanayotokea kushindwa kufanya vizuri kwanza kupata mwalimu mzuri anayethubutu kufanya mzunguko wa wachezaji , wachezaji wazuri na uongozi madhubuti,” amesema Magori.
 
Magori amesema “Lameck Lawi amekuwa tatizo tumeilipa timu na mchezaji lakini lipo kwenye mamlaka husika tuwaachie wao ndio watakaoamua, msimamo wetu kuwa tumemsajili mchezaji kutokana na mahitaji ya timu,”
 
SAKHO KURUDI SIMBA
 
Hakuna ukweli wowote juu ya Pape Sakho kurejea kwa sababu hakuwahi kumjadili ni ngumu sana kuzungumzia, Aishi Manula suala lake lipo kwenye ofisi ya Mtendaji Mkuu, Phiri Mosses alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na baada ya miezi sita tumekubaliana kumalizana kisalama na hakuna kesi itakayoenda fifa,” amesema Mjumbe huyo.
 
Ameeleza kuwa Aubin Kramo wapo kwenye mazungumzo na kuweza kuachana au kumpeleka kwa mkopo baada ya kuona msimu uliopita hakucheza msimu mzima na kuhofia kumpa presha ya mashabiki.

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Bashiri popote

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 07/18/2024