Euro - Uhispania v Ujerumani


Hakimiliki ya picha: Getty Images


Euro 2024

Robo fainali

Uhispania v Ujerumani

MHPArena

Stuttgart, Ujerumani

Ijumaa, Julai 5 2024

Muda: Saa 12:00 jioni majira ya Afrika ya Kati.

 

Uhispania hawajapoteza mechi hata moja katika mashindano ya Euro 2024 yananyoendelea

nchini Ujerumani na wanapania kuendeleza rekodi hiyo watakapokutana na wenyeji Ujerumani

kwenye mechi ya robo fanali ugani MHPArena Julai 5 Ijumaa.

 

Kwa mara ya kwanza katika mashindano ya mwaka huu 2024, La Furia Roja walitangulia

kufungwa na wapinzani baada ya Robin Le Normand kutia mpira golini pake dakika ya 18 na

kuwapa uongozi Georgia kwenye mechi hiyo ya hawamu ya 16 iliyochezwa Juni 30.

Uhispania chini ya kocha Luis de la Fuente walisawazisha katika dakika ya 39 kupitia mchezaji

Rodri kabla ya Fabian, Nico Williams na Dani Olmo kufunga goli la pili, tatu na nne katika

dakika ya 51, 75 na 83 na kunyakua ushindi wa 4-1.

 

Uhispania ambao ni mabingwa mara tatu wa kombe hili la Euro waliibuka na ushindi wa kundi B

wa asilimia 100 baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Croatia, 1-0 dhidi ya Italia na 1-0 dhidi ya

Albania.

 

Uhispania na Ujerumani walikutana kwa mara ya mwisho kwenye mechi ya makundi ya kombe

la dunia 2022 ambapo mechi hiyo iliishia sare ya 1-1, Niclas Fullkrug akifunga dakika ya 84

kusawazisha goli la Alvaro Morata la dakika ya 62.

Luis de la Fuente of Spain
Hakimiliki ya picha: Alamy 

 

Huku De la Fuente akikiri kuwa wenyeji Ujerumani ni kikosi kilicho na uwezo mkubwa na

wapinzani wenye hadhi kubwa, kocha huyo ana uhakika kikosi cha Uhispania ni bora katika

shindano la mwaka huu.

 

“Tuna uhakika na kikosi chetu kilicho jaa talanta, kinachojiamini na kinachojituma sana,”

alisema. “Ni jambo la muhimu sana unapokuwa na uhakika na uwezo wako. Sina jeuri yoyote

lakini tuna kikosi bora zaidi katika shindano hili.

 

"Kikosi cha Ujerumani ni kizuri, wanajivunia baadhi ya wachezaji bora duniani, wana

mshikamano mzuri na nidhamu ya hali ya juu. Watakutana na wapinzani walio na sifa kama

hizo; wanaojituma sana, walio na mpangilio na njaa ya kubwa ya mafanikio.

 

"Ni mambo na maamuzi ya kina wakati mwafaka yanayoamua matokeo ya mechi ya mpira wa

miguu. Ni msemo wa kawaida lakini ndio ukweli.”

 

Takwimu baina ya timu hizi mechi tano za mwisho.

Mechi - 5

Uhispania - 1

Ujerumani - 1

Sare - 3


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Bashiri popote

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 07/05/2024