AHMED ALLY: MSIMU ULIOPITA TUMECHEZEWA SANA...


Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo 


Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa msimu wa 2024/25 hawabahatishi katika suala la usajili kwa kuleta watu wenye ubora watakaowasahulisha wanasimba masimango waliyopata kwa misimu mitatu mfululizo.
 
Akizungumza na Spotileo, Ahmed amesema kutokana na masimango waliyoyapata misimu mitatu yamemuibua Mwekezaji, Mohammed Dewji kurejea kwenye nafasi ya Uenyekiti wa Bodi na kusimamia masuala yote ya usajili.
 
Amesema wanaenda kufanya usajili mkubwa kwa kugusa kila nchi kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi kwa kuziba nafasi ya wachezaji watakaopewa ‘Thank You’ .
 
“Tumeshaanza kutoa‘Thank You’ kwa wale wachezaji ambao  hatutawahitaji kwa msimu ujao, baada ya hapo tutawatangaza waliongeza mkataba na mwisho tutaweka wazi silaha zetu mpya.
 
Msimu uliopita tulichezewa sana na kupewa kila aina ya masimango hali iliyomtoa ughaibuni mwekezaji wetu kuja kushika kijiti cha usajili kwa kuhakikisha hatufanyi makosa na kuamua kuvunja Bank kwa ajili ya usajili wa nyota wapya,” amesema Ahmed.
 
Amewatuliza wanasimba na kuwataka kuwaunga mkono viongozi kwa sasa wapo sokoni kwa ajili ya kufanya usajili makini, msimu huu hawabahatishi kwa sababu ya mwekezaji huyo kutoangalia fedha na kutaka furaha ambayo anaipata pale Simba inapofanikiwa.
 
“Watakaondoka wamefanya kazi nzuri lakini hao wanaokuja ni wazuri zaidi naimani yale maneno kutoka kwa wapinzani wetu hayatakuwepo kwa sababu tunarejea katika ufalme wetu,” amesema meneja huyo.
 
Kuhusu Kocha Mkuu, Ahmed amesema hilo suala hilo lipo chini ya kamati maalum kufanyiwa kazi na anatarajia atakuja kocha mwenye kiwango kizuri na Simba kuwa salama na Agosti mwaka huu utakuwa ni mwezi wa furaha

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Bashiri popote

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 06/25/2024