WAKATI YANGA WAKIKUBALI YAISHE KWA MAYELE...KIFAA KIPYA KITAKACHOMRITHI HIKI HAPA


UONGOZI wa Yanga umesema wiki ijayo watatikisa nchini kwa kukamilisha usajili ya nyota wa kingeni ambaye atakabidhiwa jezi na Sita baada ya kukamilisha usajili ya Winga Maxi Mpia Nzengeli
 
Nzengeli amesainia mkataba wa miaka miwili kutoka Maniema Union ya Kindu, kutoka jimbo la Maniema, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).
 
Max anakuwa mchezaji mpya wa nne kuelekea msimu noya wa 2023/24, baada ya mabeki Nickson Kibabage kutoka Singida Fountain Gate, Gift Freddy kutoka Villa ya Uganda na kiungo Jonas Mkude kutoka Simba.
 
Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema wamekamilisha usajili wa winga huyo anbaye amecheza timu ya taifa ya DRC kwenye michuano ya CHAN na mchezaji bora wa nchini humo.
 
Alisema wamefanikiwa kumleta Mbappe wa DRC na mashabiki watarajie makubwa zaidi na wiki ijayo kutikisa kwa kushusha siraha nyingine anbayo atakuja kukabidhiwa jezi namba sita.
 
“Tunaenda kuboresha kikosi chetu, Max amekuja kuongeza nguvu ndani ya kikosi chetu, mashabiki waendelee kuvuta subira kwa sababu wiki ijayo ndio tutawapa furaha kwa kuendeleakushusha kifaa kitakachovaa jezi namba sita.
 
Mashabiki wasiwe na wasiwasi juu ya msimu ujao mashabiki watapata raha na tabu itabaki pale pale kwa wapinzani wetu kwa kuendelea kutetea mataji yetu,” alisema Kamwe.
 
Kuhusu mazoezi, Kamwe alisema wachezaji waliotambulishwa akiwemo Mkude tayari wameingia kambini na kuendelea na proglamu ya mazoezi kujiandaa na msimu mpya.
 
Aliongeza mazoezi hayo chini ya Kocha wao, Miguel Angel Gamondi yanaendelea vizuri kwa asubuhi kufanya mazoezi ya viungo ‘Gym' na jioni uwanjani kwa ajili ya mbinu na kucheza mpira.
 
MBADALA WA MAYELE KUTAFUTWA.
 
Uongozi wa Yanga umefikia makubaliano ya kumuuza nyota wao wa kimataifa wa DR Congo, Fiston Mayele baada ya nyota huyo kuonyesha nia ya kutaka kuondoka, huku mabingwa hao wakisaka mbadala wake wa kusaidiana na Kennedy Musonda.
 
Mayele ambaye alikuwa mfungaji bora Ligi Kuu akifunga mara 17, akiwa pia kinara wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) akifikisha mabao saba, anatakiwa na timu za AL Qadisiyah ya Saudi Arabia na Pyramids ya Misri.
 
Kwa mujibu wa taarifa ni kuwa uongozi wa Yanga umepokea ofa ya Dola
40,000 kutoka kwa moja ya timu hizo, ambayo ni suala la muda tu kumalizana na mchezaji huyo pamoja na uongozi wa timu.
 
Wakati Mayele akikaribia kuondoka Yanga, miamba hiyo ina majina manne mezani ya mshambuliaji ambaye anaweza kuvaa viatu vya mfungaji bora huyo mara mbili wa klabu, likiwamo la Makabi Lilepo wa Al Hilal ya Sudan, mwenye mkataba wa mwaka mmoja na timu yake.
 
"Mchezaji kaonyesha nia ya kuondoka na klabu ambazo zinamtaka zimefika mezani, baada ya kukaa na Mayele kwa zaidi ya mara tatu, ametuhakikishia kuwa anataka kuondoka, hivyo uongozi umeridhia hilo," alisema mmoja wa viongozi wa Yanga, jana.
 
Taarifa hizo zilisema, uongozi tayari umeweka ofa mezani juu ya Mayele, hivyo klabu inasubiri uamuzi wao kama watarudi watakuwa tayari kuondoka na nyota huyo aliyeipa Yanga mataji sita.
 
Klabu ya AL Qadisiyah, ambayo imetajwa kumhitaji Mayele, ndiyo ambayo Mtanzania Simon Msuva na nyota wa DRC, Walter Bwalya wanaitumikia.
 
Akizungumzia taarifa za kutaka kuondoka kwa nyota huyo, Rais wa Yanga, Hersi Said, alisema Mayele ni mchezaji bora na klabu hiyo ina furaha kuona akihusishwa kutakiwa na timu nyingine.
 
Hersi alisema hatua hiyo inaonyesha kuwa Yanga ni timu kubwa na ina wachezaji wakubwa ambao wanatazamwa na klabu kubwa, hivyo suala lake likiwa tayari taarifa zitatolewa, kwa sasa timu inaendelea na maandalizi ya msimu mpya.
 
“Kama atakuwa anataka kuondoka, tutaangalia vitu vitatu, moja tutataka kumbakiza, mbili tutaangalia bei nzuri, tatu ni nani atachukua nafasi yake," alisema Hersi katika moja ya mahojiano yake jijini Dar es Salaam.
 

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 

Published: 07/21/2023