PGA - 2023 John Deere Classic 


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2023 John Deere Classic 

PGA Tour 

TPC Deere Run 
Silvis, Illinois, USA 
6-9 July 2023
 
J.T Poston anatarajia kuwa mchezaji wa gofu wa nne kushinda shindano la gofu la John Deere Classic mfululizo baada ya David Frost, Deane Beman na Steve Stricker.
 
Kuhusu Poston
 
Mchezaji huyu raia wa Marekani ameshinda mashindano mawili tangu kuanza kucheza gofu ya kulipwa mwaka 2016 huku mashindano yote mawili yakiwa ni sehemu ya PGA Tour. 
 
Poston alishinda shindano la kwanza la gofu aliposhiriki shindano la Wyndham Championship mwaka 2019.
 
Cha kufahamu
 
J.T Poston mwenye jina la utani Postman hakupata nafasi ya kushiriki shindano la 2023 la Travellers Championship. Alichukua mapumziko kutoka mchezo wa gofu hivyo basi kukosa shindano la 2023 la Rocket Mortgage Classic. 
 
The Postman anashikilia nafasi ya 62 kwenye jedwali rasmi la gofu duniani sasa hivi. Mchezaji huyo aliwahi kushika nafasi ya 47 kwenye jedwali la ubora duniani. 
 
Poston ni miongoni mwa wanaopigiwa upatu ksuhinda. 
 
Poston aliibuka na ushindi wa shindano la John Deere Classic 2022 alipowabwaga Christiaan Bezuidenhout na Emiliano Grillo baada ya kuongoza katika kila awamu ya shindano hilo. 
 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 aliweka rekodi ya kuwa mshindi wa kwanza tangu mwaka 1992 kushinda shindano hili baada ya kuongoza kila awamu ya shindano. 
 
Nukuu
 
“Sio rahisi. Kuongoza kila awamu ya shindano kutoka mwanzo hadi mwisho sio rahisi. Siachi kuwaza juu yake,” alisema Poston baada ya kushinda the John Deere Classic.
 
"Nilizangatia sana mbinu. Haikuwa rahisi. Hali hii ilikuwa ngumu kuliko hata siku za kwanza. Nilijikaza sana. 
 
"Nikitathmini hali ya leo na wiki hii, nahisi nina uwezo wa kupambana na changamoto na shinikizo na kuibuka na ushindi.” 
 

Washindi watano wa mwisho wa John Deere Classic.

 
2017- Bryson DeChambeau (Marekani)
2018 - Michael Kim (Marekani)
2019 - Dylan Fritteli (Afrika ya Kusini)
2021 - Lucas Glover (Marekani)
2022 - J.T Poston (Marekani)
 

Bashiri Gofu na Betway

Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 

Published: 07/05/2023