NBA - Safari ya Nuggets kutwaa taji la NBA


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 National Basketball Association (NBA) season

Number of games 82

Number of teams 30
Canada and USA
18 October 2022 - 12 June 2023
 
Denver Nuggets ni mabingwa wa ligi ya mpira wa kikapu, National Basketball Association (NBA) msimu 2022/23 ikiwa ni taji lao la kwanza katika historia ya timu hiyo.
 
Safari yao kuelekea michuano ya mchujo.
 
The Nuggets walifuzu kushiriki mechi za mchujo baada ya kumaliza katika nafasi ya kwanza kwenye michezo ya Western Conference.
 
Timu hiyo kutoka Denver ilipata kushinda mechi 53 na kupoteza michezo 29 katika jumla ya michezo  82 chini ya mwalimu Michael Malone.
 
Ushindi huu unawakilisha asilimia 64.6.
 
Safari yao kufika fainali.
 
The Nuggets iliishinda Minnesota Timberwolves jumla ya 4-1 kwenye mechi za awamu ya kwanza za Western Conference kabla ya kuwaondoa Phoenix Suns 4-2 hatua ya nusu fainali.
 
Denver Nuggets chini ya mkufunzi Malone walionyesha ukakamavu katika fainali ya michezo ya Western Conference dhidi ya Los Angeles Lakers wakiongozwa na mchezaji nyota LeBron James walipoibuka na ushindi wa 4-0.
 
Walitawazwa ubingwa wa ligi hiyo baada ya kuwashinda Miami Heat 4-1 kwenye fainali ya michuano ya muondoano.  
 
Wachezaji muhimu
 
Nikola Jokic na Jamal Murray wa the Nuggets walionyesha ueledi wao wa kusakata mchezo huo kwenye mechi ya fainali uliochangia pakubwa kuwapa ubingwa.
 
Jamal Murray aliingia kwenye orodha ya pamoja na James, Magic Johnson na Michael Jordan kama wachezaji wa pekee kwenye historia kufikia wastani wa alama 20 katika mchezo mmoja wa misururu ya fainali.  
 
Jokic alionyesha viwango vya juu msimu wote, juhudi zilizopelekea yeye kuteuliwa kwenye tuzo za mchezaji bora wa ligi wa msimu (MVP).
 
Nukuu
 
"Bado tuna uchu wa mafanikio zaidi,” alisema Malone baada ya kuwa mkufunzi wa kwanza wa Nuggets kushinda taji la NBA.
 
"Tumepata mafanikio ambayo hayajawai kupatikana awali na timu hii. Tunao wachezaji wachanga na wenye talanta miongoni mwetu.
 
"Tumedhihirisha uwezo wetu kuwa tunaweza kukabiliana na upinzani wa kiwango cha juu kwa kushinda mechi 16 za msururu wa michezo ya muondoano.”
 
Mabingwa wa NBA - Denver Nuggets
 
Mchezaji bora wa NBA - Joel Embiid
 
Mchezaji bora wa fainali za NBA - Nikola Jokic 
 
Mkufunzi bora wa msimu wa NBA - Mike Brown
 

Bashiri Mpira wa Kikapu na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.




Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 
 

Published: 07/07/2023