Hakimiliki ya picha: Soka la Bongo
Mchambuzi mahiri wa soka, Saleh Ally Jembe amesema
Klabu ya Simba imemvumilia sana aliyekuwa mchezaji wake, Jonas Mkude kutokana na matukio mbalimbali ya utovu wa nidhamu aliyokuwa akiyafanya.
Jembe amesema kuwa hata ikitokea Mkude ameenda Yanga, kwake anaona ni sawa kwa sababu mchezaji anao uhuru wa kuchagua timu anayoitaka lakini akatahadharisha kwamba anatakiwa kujirekebisha kwa sababu siyo klabu zote zinazoweza kuvumilia matatizo yake.
“Mkude kwenda Yanga au asiende huo ni uamuzi wake, ana haki ya kucgaua pa kwenda, cha pili nisema Simba hawapaswi kujuta kumpoteza Mkude kwa kuhofia mashabiki.
“Ukiwa kiongozi ukawa unahofia mashabiki, basi unatoka kwenye sifa za kuwa kiongozi bora, badala yake kiongozi unatakiwa uangalie usahihi wa jambo unaloliamua hata kama watu wote hawakuungi mkono.
“Ukiangalia kwa misimu miwili msaada wa Mkude kwa Simba ulikuwa chini sana, na sisi waandishi wa habari tunajua na tumesikia mambo mengi ya ndani ambayo ukiangalia klabu ndiyo ilikuwa ikimvumilia mkude.
“Nashangaa watu wanasema kwa nini Mkude hajaagwa? Unajiuliza kwa kipindi hiki (likizo ya msimu) Simba waandae mechi wakusanye wachezaji kwa ajili ya kufanya sherehe ya kumuaga Mkude? Hilo nadhani litafanyika kwenye Simba Day.
“Lakini najiuliza kwa nini Mkude naye asiwafanyie sherehe Simba? Kwa sababu walimlea, wakamvumilia kwa mambo mengi sana. Mkude akienda Yanga hakuna shida yoyote, lazima kuna vitu atatakiwa abadilike, maana si kila mtu atamvumilia tabia yake,” amesema Jembe.
SIMBA KUACHA WENGINE ZAIDI
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema wiki hii watakamilisha zoezi la kuagana na wachezaji ambao hawataendelea nao msimu ujao Ahmed amesema klabu bado iko kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji ambao wengine watawasitishia mikataba yao kwa kuwa hawamo katika mipango ya Kocha Robertiho Oliveira katika msimu ujao.
"Bado hatujafunga zoezi la kuagana na baadhi ya wachezaji, tuko kwenye mazungumzo ya kusitisha mikataba ya wachezaji ambao hawatakuwa nasi msimu ujao"
"Tunatarajia zoezi hili tutalikamilisha wiki hii ili wiki ijayo tuanze kutambulisha wachezaji tuliowasajili kuchukua nafasi za wachezaji walioachwa," alisema Ahmed.
Wachezaji ambao mpaka sasa wamepewa mkono wa kwaheri na klabu ya Simba ni Augustine Okrah, Victor Akpan, Nelson Okwa na Mohammed Ouattara.
Wengine ni Beno Kakolanya, Erasto Nyoni na Jonas Mkude.
BOCCO AZIGONGANISHA TIMU HIZI.
Wakati kwenye vikao vya Simba vikiendelea kujadili jina la nahodha wao, John Bocco kama wanaweza kuendelea naye ama kuachana naye, kuna timu zinasubiri baibai yake tu ili zimnyakue.
Simba ilimuomba Bocco apewe jukumu lingine (umeneja), lakini hakuwa tayari kustaafu.
Wakati hayo yanaendelea, inatajwa Singida Big Stars inaandaa fungu la maana kupata saini ya Bocco, timu nyingine ni Ihefu na Namungo FC.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.