HUKU ISHU YA CHAMA IKIZIMWA KIMYA KIMYA...MBRAZILI ASHINDWA KUJIZUIA KUHUSU MASTAA WAPYA


Hakimiliki ya picha: Soka la Bongo


KOCHA mkuu wa Simba, Mbrazil, Robert Oliveira 'Robertinho' ameuambia uongozi wa timu huyo kuhakikisha anawapata wachezaji wote wapya wenye kuivusha timu hiyo  kimataifa kwa kupanda viwango kutoa  saba hadi tatu.
 
 
Robertinho ametoa kauli hiyo kufuatia baadhi ya nyota wapya waliosajiliwa ndani ya kikosi hicho kushindwa kulipoti kwa wakati katika kambi ya timu hiyo iliowekwa nchini Uturuki akiwemo Miquissone ambaye usajili wake bado unashughulikiwa na mabosi wa timu hiyo.
 
 
Tayari Simba kwa sasa inashughulia safari ya Willy Essomba Onana, Che Fondoh Malone Jean Baleke na Fabrice Ngoma ametambulishwa jana kabla ya kuelekea katika kambi  jumatatu ya Julai 17,  2023.
 
 
  Kocha Robertinho alisema msimu ujao wanatarajia kushiriki mashindano mengi ikiwemo Super League ambayo ni muhimu kufanya vizuri na kutakiwa kufanya usajili wa wachezaji wenye kiwango kuwavusha na kufikia malengo yao.
 
 
Alisema  mashindano  makubwa kwa sababu ya timu kubwa zinashiriki  Super League,  Simba inahitaji kufanya vizuri na kuendelea kufanya usajili mkubwa kwa kila nafasi ikiwa na zaidi ya wachezaji wawili.
 
 
“Usajili ni mzuri na wachezaji wenye kiwango kizuri ambao watafikia malengo yao, Simba iko ndani ya 10 bora katika viwango vya Fifa ni jambo la kujivunia hii inatokana na uwezo mkubwa wa wachezaji wazuri na kufanya vizuri katika michuano.
 
 
Sasa tunahitaji wachezaji wazuri jambo ambalo linafanyika kwa viongozi wangu kukamilisha usajili na kujiunga na timu katika maandalizi yetu ya msimu ujao,” alisema Robertinho.
 
 
Aliongeza kuwa Simba inaendelea kufanyza mazoezi kwa awamu mbili asubuhi na jioni, anafurahi mazingira mazuri ya kambi kwa kufanya program ya mazoezi kwa umakinj.
 
 
Kocha huyo alisema mazoezi ya asubuhi yalikuwa mapesi kwa wachezaji kuwek miili zoezi hili likisimamiwa na kocha wa viungo Corneille Hategekimana walianza kukimbia nusu uwanja kabla ya kuanza ya viungo ikiwemo kutumia vifaa mbalimbalu kama fimbo fupi za kuruka na koni.
 
 
Alisema mazoezi ya jioni yalikuwa ya nguvu, mbinu na ufundi kwa kucheza mpira aina tofautu na muda mwingi alikuwa akilenga kwenye eneo la ufundi huku yakisimamiwa ipasavyo na wasaidizi wake.
 
 
“Imekuwa bahati kwa upande wangu  kwa kuwa wachezaji wapo kwenye hali nzuri na utimamu kwa sababu kila aina ya mazoszi aliyopanga wafanye wametimiza kwa ufanisi kitu ambacho amekifurahia.
 
 
Tumeanza vizuri mazoezi, siku zinavyozidi kwenda tutakuwa tunabadilisha mbinu mbalimbali. Jambo zuri kwangu kuona wachezaji wote wanahamu ya kufa kila ambacho anahitaji kutoka kwao,” alisema Robertinho.
 
 
Kikosi cha Simba kipo  Uturuki na kimeanza maandalizi ya msimu wa mashindano 2023/24 ikiwemo michuano ya Super League ambayo inashirikisha timu nane ambazo ni Ahly ya Misri, Wydad Casablanca ya Morocco, Esperance ya Tunisia
 
 
Nyingine ni  Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, TP Mazembe ya DR Congo, Enyimba ya Nigeria,  Petro Atletico ya Angola na Simba inaendelea na mazoezi katika uwanja wa Soguksu Sports complex.
 

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 

Published: 07/21/2023