Hakimiliki ya picha: Getty Images
2023 Formula One World Championship
2023 British Grand Prix
Round 10
Silverstone Circuit
Silverstone, England
Sunday, 9 July 2023
Mbio za 2023 za
British Grand Prix zimepangiwa kufanyika katika mkondo wa Silverstone, Silverstone, England Julai 9.
Historia ya mbio hizi.
British Grand Prix iliandaliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1926 na mbio hizi zimekuwa zikiandaliwa kila mwaka tangu mwaka 1948 na zimekuwa kwenye msururu wa dunia wa Formula one kila mwaka tangu 1950.
British Grand Prix ni mbio za zamani kabisa kwenye ratiba ya mashindano ya dunia ya Formula One kwani mkondo wa Silverstone uliandaa mbio za kwanza za msimu wa F1 mwaka 1950.
Mbio za hivi karibuni
Mkondo wa tisa wa msimu huu wa F1 ulikuwa mbio za Austrian MotoGP ambao ulifanya Julai 2. Max Verstappen wa Red Bull Racing-Honda RBPT aliibuka na ushindi wa mbio hizo.
Dereva wa Ferrari Charles Leclerc na Sergio Perez wa Red Bull Racing-Honda RBPT walimaliza katika nafasi ya pili na tatu mtawalia kwenye mbio hizo zilizoandaliwa Red Bull Ring, Spielberg.
Msimamo.
Verstappen anazidi kuongoza kwenye jedwali la dunia la madereva akifuatiwa na Perez katika nafasi ya pili huku Alonso akichukua nafasi ya tatu.
Kampuni ya Red Bull Racing-Honda RBPT inachukua nafasi ya kwanza kwenye jedwali la waundaji ikifuatiwa kwa karibu na Mercedes huku Aston Martin Aramco-Mercedes ikichukua nafasi ya tatu mtawalia.
Wanaopigiwa upatu kushinda.
Inatarajiwa kuwa Verstappen ataibuka na ushindi wa mbio za British Grand Prix kwani amekuwa na msururu wa matokeo mazuri huku akifanikuwa kushinda mbio tano za msimu huu mfululizo.
Hata hivyo, Verstappen atakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa Perez, Leclerc, Alonso na Lewis Hamilton ambaye ni mshindi mara nane wa mbio za British Grand Prix.
Nukuu
"Zipo siku ambazo nafurahia kazi yangu na siku zingine ambazo nahisi ningefanya juhudi zaidi kama ilivyo leo,” alisema Hamilton baada ya kumaliza katika nafasi ya nane kwenye mbio za Austrian Grand Prix 2023.
"Muda mwingine katika mbio unahisi kuishiwa na nguvu na kuzidi kupambana. Inashangaza sana upande wetu kwani siku moja tufanya vizuri sana na wakati mwingine tunakuwa na matokeo ya ovyo.
"Iwapo unajali unachokifanya inakubidi utupilie mawazo hayo ya kukata tamaa mbali na unazidi kupambana. Nimejiandaa vizuri kwa ajili ya mkondo wa Silverstone, nyumbani.”
Matokeo ya mbio za 2022 British Grand Prix.
Mshindi: Carlos Sainz Jr - Ferrari
Nafasi ya pili: Sergio Perez - Red Bull Racing-RBPT
Nafasi ya tatu: Lewis Hamilton - Mercedes
Bashiri Motosport na Betway
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni soka, motorsport, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.