Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 Rocket Mortgage Classic
US PGA Tour
Detroit Golf Club
Detroit, Michigan, USA
28-31 July 2022
Shindano la gofu la
Rocket Mortgage Classic 2022 linatarajiwa kung’oa nanga Detroit Golf Club, Detroit Marekani kati ya tarehe 28 na 31 Julai.
Shindano hili liliandaliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2019 na kuwa mbadala wa shindano la gofu la awali la Quicken Loans National kwenye ratiba ya PGA Tour.
Mfadhili wa shindano hilo ni kampuni ya Rocket Mortgage LLC, zamani ikiitwa Quicken Loans LLC na ambayo ni kampuni ya rehani yenye makao makuu Detroit.
Shindano la gofu la Rocket Mortgage Classic ni shindano la kwanza la PGA katika histori kuandaliwa ndani ya mipaka ya mji wa Detroit.
Cameron Davis ndiye bingwa wa sasa wa shindano hilo baada ya kushindano la mwaka jana alipowashinda Troy Merritt na Joaquín Niemann kwenye mechi za mchujo.
Davis anatajia kutetea taji lake kwa mafanikio mwaka huu lakini atakumbana na upinzani mkali kutoka kwa wachezaji kama Patrick Cantlay, Will Zalatoris, Tony Finau na Cameron Young.
Max Homa, Kevin Kisner, Trey Mullinax, Harris English, Adam Scott na Cameron Tringale vile vile watakuwa miongoni mwa washiriki wa shindano hilo ambalo litakuwa na wachezaji 156 na litakalochezwa ndani ya siku nne.
Zawadi ya shindano hili ni dola za kimarekani milioni 8.4 huku wachezaji tisa waliopo hamsini bora kwenye jedwali la dunia wakipigiwa upatu kushinda shindano hili.

Hakimiliki ya picha: Getty Images
Mkurugenzi mtendaji wa Rocket Mortgage Classic Jason Langwell alieleza kuwa hana wasiswasi wowote kushindana na shindano la LIV Golf Invitational Series wiki hii.
"Hatuna wasiwasi wowote. Tuna imani na kazi yetu. Shindano letu haliwezi kulinganishwa na lingine. Tuna furaha kubwa kuhusu shindano hili na wachezaji watakaoshiriki kuwa sehemu ya historia yake,” alisema Langwell.
"Ushirikiano wetu na PGA Tour unahusisha kuwashirikisha wachezaji wakubwa wa gofu kama vile Bryson DeChambeau kuwa mabalozi wa Rocket Mortgage.
"Kama inavyofahamika, Bryson alichagua kujiunga na LIV Golf Series. Kuanzia muda huu, kampuni ya Rocket Mortgage imesitisha makubaliano ya udhamini na Bryson. Tunamtakia kila la kheri."
Washindi watatu wa mwisho wa shindano la Rocket Mortgage Classic
2019 - Nate Lashley - Marekani
2020 - Bryson DeChambeau - Marekani
2021 - Cameron Davis - Australia
Bashiri Gofu na Betway
Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.