Man United na Liverpool kukutana Thailand


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 Football Pre-Season 

Club Friendly

Manchester United v Liverpool FC 

Rajamangala National Stadium 
Bangkok, Thailand 
Tuesday, 12 July 2022
Kick-off is at 4 pm  
 
Manchester United na Liverpool FC watamenyana kwenye mechi kubwa ya kirafiki ya kujiandaa kwa msimu ujao, katika uga wa kitaifa wa Rajamangala Julai 12. 
 
The Red Devils walimaliza msimu 2021-22 kwa kupoteza mechi yao ya mwisho ya ligi ya premier 1-0 ugenini dhidi ya Crystal Palace mnamo Mei 22.
 
Hivyo basi, United hawajashinda mechi yoyote katika mechi mbili za mwisho katika mashindano yote huku wakishindwa mechi zote mbili ikiwa pamoja na kuchapwa 4-0 dhidi ya Brighton and Hove Albion.
 
Kwengineko, Liverpool walimaliza msimu 2021-22 kwa kushindwa 1-0 na Real Madrid ya Uhispania katika fainali ya ligi ya mabingwa, UEFA Champions League mnamo Mei 28
 
Kabla ya mechi hiyo, The Reds walikuwa hawajapoteza mechi yoyote katika mechi 18 kwenye mashindano yote huku wakiandikisha ushindi mara 15 na sare 3.
 
Mlinzi wa Liverpool Rhys Williams amesema kuwa wanataka kuonyesha mkufunzi wao mchezo mzuri watakapoikabili United.  
 
“Wachezaji wote wanataka kucheza na kucheza vizuri. Inafurahisha kucheza na United kwenye mataifa ya ugenini na pia kushuhudia utamaduni wa maeneo haya,” alisema Williams. 

Marcus Rashford of Manchester United
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
“Unapata wakati wa kuona vivutio vipya na sehemu mpya ambazo sio kawaida kutembelea kipindi cha mapumziko ya msimu. Ni vizuri kutembelea maeneo haya. Iwapo kocha atahitaji nibaki kwenye timu baada ya kuonyesha mchezo mzuri nitafurahi. 
 
"Iwapo nitacheza sehemu nyingine, sharti nionyeshe uwezo wangu kwenye mechi kubwa hata kama ni za kirafiki kwa sababu ni mechi kubwa dhidi ya timu kubwa za ligi ya premier.” 
 
Hii itakuwa mechi ya 210 baina ya timu hizi mbili tangu mechi ya kwanza ilipochezwa Oktoba 12 1895. 
 
United inaongoza kwa kushinda mchuano huu baina ya timu hizi huku ikishinda mara 81 na Liverpool ikishinda mara 70. Sare zimekuwa 58.
 

Takwimu baina ya timu hizi

 
Mechi - 209
Man United - 81
Liverpool - 70
Sare - 58


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 07/11/2022