Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 Genesis Scottish Open
US PGA Tour
European Tour
The Renaissance Club
North Berwick, Scotland
7-10 July 2022
Shindano la gofu la
Genesis Scottish Open mwaka 2022 linatarajiwa kung’oa nanga Renaissance Club North Berwick nchini Scotland kati ya tarehe 7 na 10 Julai.
Shindano hili liliasisiwa mwaka 1972 na ni moja kati ya mashindano matano ya msururu wa Rolex ambalo ni shindano kubwa kwenye European Tour.
Kuanzia mwaka 2022, shindano hili litaandaliwa kwa pamoja na PGA Tour na taji litadhaminiwa na Genesis ambayo ni sehemu ya kiwanda cha gari cha Korea Kusini kiitwacho Hyundai.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Min Woo Lee ndiye bingwa mtetezi wa shindano hilo baada ya kushindano la 2021 la Scottish Open alipowashinda Thomas Detry na Matt Fitzpatrick kwenye mzunguko wa muondoano.
Shindano la mwaka huu litakuwa moja ya shindano kubwa katika historia ya Scottish Open kwani litajumuisha wachezaji wakubwa wa DP World Tour na PGA Tour wakipambana ikiwa mara ya kwanza shindano kuandaliwa kwa pamoja.
Kati ya washiriki 156 watakuwa wachezaji Woo Lee, Jon Rahm, Collin Morikawa, Scottie Scheffler, Sam Burns, Billy Horschell, Danny Willett, Francesco Molinari na Justin Thomas.
Zawadi ya shindano hili itakuwa dola milioni nane na wachezaji wanaoshikilia nafasi 31 za kwanza kati ya 50 bora duniani wanapigiwa upatu kushinda shindano lenyewe.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
“Nilifurahia juma la shindano la Scottish Open mwaka jana,” alisema Scheffer ambaye anashikilia nafasi ya kwanza kwenye jedwali rasmi la dunia.
"Nina furaha kushiriki shindano hilo Renaissance Club mwezi Julai. Zitakuwa wiki mbili za kusisimua nchini Scotland.
“Nilikuwa nimepata habari nyingi kuhusu shindano lenyewe na msururu wa shindano la Rolex kabla sijashiriki mara ya kwanza na sifa hizo zilikuwa za kweli. Mengi yametokea kutoka kipindi hicho.
"Natarajia kuwa na mchezo mzuri majira yajayo.”
Ian Woosnam ndiye mchezaji aliye na mafanikio makubwa katika historia ya shindano la Scottish Open ikiwa ameshinda mara tatu.
Washindi watano wa mwisho wa Scottish Open
2017 - Rafa Cabrera-Bello – Uhispania
2018 - Brandon Stone – Afrika Kusini
2019 - Bernd Wiesberger - Austria
2020 - Aaron Rai - Uingereza
2021 - Min Woo Lee - Australia
Bashiri Gofu na Betway
Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.