Macho yote yaangazia mbio za 2022 za Hungarian Grand Prix


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 FIA Formula One World Championship 

13 Round

2022 Hungarian Grand Prix

Hungaroring
Mogyoród, Hungary.
Sunday, 31 July 2022
 
Mbio za langalanga za 2022 za Hungarian Grand Prix zinatarajiwa kuandalliwa Julai 31 Mogyoród ambao ni mji mdogo wa kitamaduni uliopo Manispaa ya Pest nchini Hungury
 
Hizi zitakuwa ni mbio za 13 za Formula One msimu wa 2022 na zitafanyika katika mkondo wa Hungarong ambapo mbio za Hungarian Grand Prix zimekuwa zikiandaliwa tangu mwaka 1986.
 
Mbio za kwanza za Hungarian Grand Prix ziliandaliwa Juni 21 mwaka 1936 Népliget nchini Budapest. Hata hivyo, hali ya kisiasa na vita vilipelekea kusitishwa kwa mbio hizo nchini humo kwa miaka hamsini.
 
Mbio za langalanga za hivi karibuni za msimu wa 2022 wa Formula One zilikuwa French Grand Prix mnamo Julai 24 na Max Verstappen aliibuka na ushindi.

Carlos Sainz JrHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Madereva wa Mercedes Lewis Hamilton na George Russell walimaliza katika nafasi ya pili na tatu mtawalia huku timu ya Mercedes-AMG Petronas F1 ikifurahia matokeo hayo nchini Ufaransa. 
 
Verstappen anasalia kileleni mwa jedwali la madereva msimu huu wa 2022 akiwa na alama 233 huku akipania kutetea taji lake la Formula One kwa mafanikio.
 
Dereva wa Ferrari Charles Leclerc akiwa na alama 170 na dereva wa Red Bull Racing-RBPT Sergio Perez akiwa na alama 163 wanashikilia nafasi ya pili na tatu mtawalia huku zikiwa zimesalia mbio kumi msimu huu kukamilika.  
 
Carlos Sainz wa Ferrari na alama144, Russell na alama 143 na Hamilton akiwa na alama 127 wanashikilia nafasi ya nne, tano na sita mtawalia katika jedwali.  

George RussellHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
"Tunaendelea vizuri sana lakini tunahitaji kuimarisha matokeo yetu katika kufuzu kwa sababu hatujaonyesha juhudi endelevu. Tunafahamu tatizo letu kama timu ni magurudumu. Ni tatizo lililonikumba mwanzoni mwa mbio,” alisema Rusell baada ya mbio za French Grand Prix.
 
"Kasi yetu leo ilikuwa nzuri na tunazidi kuimarika. Tunafanya kila tuwezalo kuimarisha utenda kazi wa gari letu na tuna imani tunapiga hatua. Tunasubiri kuona tutafanikiwa nini kwenye mbio zijazo.
 
"Tunazidi kuimarika na kuna nafasi zaidi ya kufanya hivyo. Tunashukuru kila mmoja kwenye kiwanda cha Brackley na Brixworth kwa umakini wa kazi yao.”
 
Kampuni ya Red Bull Racing-RBPT inaongoza kwenye jedwali la waundaji huku wakifuatiwa na Ferrari na Mercedes mtawalia.
 

Matokeo ya 2021 ya mbio za Hungarian Grand Prix

 
Mshindi: Estaban Ocon- Alpine Renault 
Nafasi ya pili: Lewis Hamilton - Mercedes 
Nafasi ya tatu: Carlos Sainz Jr - Ferrari 
 

Bashiri Motosport na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 

Published: 07/28/2022