Macho yote yaangazia 3M Open


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 3M Open 

US PGA Tour 

TPC Twin Cities
Blaine, Minnesota, USA 
21-24 July 2022 
 
Shindano la gofu la 3M Open 2022 linatarajiwa kung’oa nanga TPC Twin Cities, Blaine, Minnesota, Marekani kati ya Julai 21 na 24.
 
Shindano hilo lilichezwa kwa mara ya kwanza kati ya Julai 4 na 7 mwaka 2019, baada ya kutangazwa na PGA Tour mwezi Juni mwaka 2018. 
 
Shindano hilo linafadhiliwa na kikundi cha kampuni za kimataifa cha Marekani 3M chenye makao yake Minnesota.
 
Shindano hili lilichukua nafasi ya 3M Championship ambalo ni shindano la PGA Tour kwa miaka 26 (1993–2018) lililokuwa likichezewa TPC Twin Cities tangu mwaka 2001.

Chez ReavieHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Bingwa wa sasa wa shindano hili ni Cameroon Champ aliyeshinda shindano la mwaka jana alipowapiku Louis Oosthuizen, Charl Schwartzel na Jhonattan Vegas kwenye mzunguko wa mchujo.
 
Miongoni mwa washiriki wa mwaka huu ni pamoja na Champ, Hideki Matsuyama, Tony Finau, Sungjae Im, Jason Day, Rickie Fowler, Tom Hoge, Chez Reavie na wengineo.
 
Shindano hili litakuwa na wachezaji 144 na litachezwa kwa zaidi ya siku nne huku wachezaji watano walio kwenye 50 bora ya jedwali rasmi la dunia wakipigiwa upatu kushinda. 
 
Zawadi ya pesa itakayoshindaniwa ni dola milioni 7.5 za kimarekani. Zaidi, mshindi wa 2020 wa shindano hili Michael Thompson atakuwa mshiriki. 

Tony Finau in action
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Angus Flanagan wa Minnesota atakuwa akishiriki shindano la 3M Open kwa mwaka wa pili mfululizo. 
 
“Hii ni kama ndoto ,” alisema Flanagan ambaye amekuwa mchezaji wa kulipwa tangu mwanzoni mwa majira haya ya joto baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu cha Minnesota. 
 
“Vile vile ilikuwa ndoto nilipokuwa naanza lakini sasa hivi kuna makubwa ya kushindaniwa. Nahitaji kutulia na kufurahia mchezo. 
 
"Nina vifaa vyangu mfukoni na naenda kucheza kwa tabasamu kisha tutaona tutafikia kiwango gani.” 
 

Washindi watatu wa mwisho wa shindano la gofu la 3M Open

 
2019 - Matthew Wolff - Marekani
2020 - Michael Thompson - Marekani  
2021 - Cameron Champ - Marekani 

 

Bashiri Gofu na Betway

Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

 

Published: 07/20/2022