Liverpool wapania kushinda taji la 16 la Community Shield


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 FA Community Shield

Liverpool v Manchester City

King Power Stadium
Leicester, England
Saturday, 30 July 2022
Kick-off is at 18h00  
 
Liverpool wanapania kushinda taji la Community Shield kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2006 watakapokutana na Manchester City ugani King Power Stadium Jumamosi Julai 30. 
 
Uwezekano wa Liverpool kushinda mataji matatu Uingereza yaliingia dosari baada ya City kushinda ligi la premier mbele yao kwa alama moja tu huku wakiridhika na kombe la FA na EFL. 
 
Machungu zaidi yalifuata vijana wa Jurgen Klopp wiki moja baadaye walipopoteza fainali ya ligi ya mabingwa 1-0 dhidi ya Real Madrid.  

Jurgen Klopp
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Vile vile, The Reds walishiriki kombe la Community Shield mwaka 2019 na 2020 lakini walipoteza safari zote dhidi ya City na Arsenal mtawalia kwa njia ya penalti. 
 
Manchester United (21) na Arsenal (16) ni timu za pekee kushinda kombe hili mara nyingi kuliko Liverpool ambao wanapania kushinda taji lao la 16 kwenye mechi hii ya kufungua msimu mpya. 
 
Licha ya kufanya vizuri na kukosa taji moja tu kati ya mataji matatu makubwa Uingereza, meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anasema kwamba bado wana nafasi ya kuimarika na kushinda ligi ya premier msimu ujao. 
 
Akizungumzia mafanikio yao ya msimu 2021/22, raia huyo wa Ujerumani aliiambia Premier League Productions kwamba timu ilicheza vizuri sana lakini kuna nafasi ya kuimarika zaidi. 
 
"Tulifanya vizuri kadri ya uwezo wetu msimu uliopita. Matokeo yangekuwa tofauti kidogo lakini uchezaji wetu ulikuwa mzuri sana. Nilifurahishwa na mambo mengi lakini tunayo nafasi ya kuimarika na tunalifanyia kazi. 
 
"Sio tu kwa sababu tunataka kuimarika bali ni sharti kuimarika kwa sababu makundi mengine yanajiandaa vilivyo. Sharti tujiandae kwa ajili ya mechi kila mwisho wa juma.” 
 

Takwimu baina ya timu hizi katika mechi tano za mwisho  

Mechi - 5
Liverpool - 1
Man City - 1
Sare - 3


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 07/28/2022