Day kufuata nyanyo za wenzake kwenye John Deere Classic


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 John Deere Classic 

US PGA Tour 

TPC Deere Run 
Silvis, Illinois, USA 
30 June - 3 July 2022 
 
Jason Day anapania kufuata nyayo za wachezaji kutoka taifa lake John Senden na Mark Hensby kwa kushinda shindano la gofu la John Deere Classic 2022.
 
Senden na Hensby wanasalia kuwa wachezaji pekee kutoka Australia kuwahi kushinda shindano hili mwaka 2006 na 2004 mtawalia.
 
Day ambaye ni mchezaji nambari moja duniani wa zamani kwenye jedwali rasmi la gofu, anatarajia kuwa mchezaji wa tatu kutoka taifa hilo kushinda shindano hilo.

Geoff OgilvyHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Mchezaji huyo mwenye makao yake Ohio alishinda shindano lake la dunia (WGC) ambalo ni WGC-Accenture Match Play Championship mnamo mwaka 2014 na kulishinda kwa mara ya pili mwaka 2016.
 
Kwa ushindi wake 2016, Day alijiunga kwenye orodha ya Tiger Woods na Geoff Ogilvy ambao ni washindi wa shindano hilo zaidi ya mara moja na kujitambulisha kama mmoja wa wachezaji wazuri wa gofu duniani.
 
Day alishinda shindano kubwa la kwanza kwenye PGA Championship mwaka 2015 na kuchukua nafasi ya tatu kwenye jedwali rasmi la gofu duniani.
 
Taji la mwisho la PGA Tour la mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 lilikuwa mwaka 2018 aliposhinda shindano la Wells Fargo Championship na ana imani atamaliza ukame wa mataji kwenye shindano la TPC Deere Run.

Tiger Woods
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
“Ndio nina imani. Ni mwelekeo mzuri,” alisema Day kwenye shindano la hivi majuzi la Wells Fargo Championship alipomaliza katika nafasi ya kumi na tano.
 
“Nitajipigia makofi kwa sababu nilicheza mchezo mzuri leo.
 
"Lakini tuna siku tatu zaidi baada ya leo na lengo kubwa ni kumakinika na kujiweka katika nafasi ya kupata ushindi. Leo ilikuwa siku ya kufana.”
 
D.A Weibring na Steve Stricker ndio wachezaji wenye mafanikio makubwa katika historia ya shindano la John Deere Classic wakiwa wameshinda mara tatu kila mmoja.
 

Washindi watano wa mwisho shindano la John Deere Classic

 
2016 - Ryan Moore - Marekani 
2017 - Bryson DeChambeau - Marekani
2018 - Michael Kim - Marekani
2019 - Dylan Frittelli – Afrika Kusini
2021 - Lucas Glover - Marekani
 

Bashiri Gofu na Betway

Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 
 

Published: 07/01/2022