Arsenal watazamia ushindi mwingine kwenye mechi ya kirafiki


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2022 Florida Cup

Arsenal v Chelsea

Camping World Stadium
Orlando, United States
Sunday, 24 July 2022
Kick-off is at 02h00  
 
Arsenal wataendelea na maandalizi ya msimu ujao watakapokutana na maasidi wao wa ligi ya premier, Chelsea, katika kombe la Florida Jumapili Julai 24.
 
The Gunners walianza mechi za kirafiki kwa ushindi wa 5-3 dhidi ya Nurnberg wakati wa kambi ya mazoezi nchini Ujerumani kanla ya kuishinda Everton 2-0 kule Baltimore katika mechi yao ya kwanza ya Marekani.
 
Sajili mpya kutoka Manchester City, Gabriel Jesus alifunga goli katika kila mechi na kuanza maisha ugani Emirates kwa juhudi nzuri.

Gabriel-Jesus.jpg
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Msimu uliopita, kila timu ilipata ushindi mmoja baina yao kwenye mechi za ligi; Chelsea ilipata ushindi wa 2-0 ugenini Agosti 22 kabla ya Arsenal kulipiza kisasi kwa ushindi wa 4-2 ugani Stamford Bridge Aprili 20.
 
Katika mechi tano za mwisho zilizopita baina yao, Arsenal imeshinda mechi tano kati ya mechi kumi walizocheza huku Chelsea ikishinda mechi nne.
 
Arteta amefurahishwa na uchezaji mzuri wa mshambuliaji Jesus na anatamani kuona makali atakayoonyesha pindi akizoeana na wachezaji wengine kikamilifu.
 
"Anatengeneza nafasi sana na kuhangaisha walinzi muda wote,” Arteta alisema baada ya ushindi dhidi The Toffees. “Wakati wote yupo kukunyang’anya mpira na kutafuta uso wa goli.
 
"Jesus ni tishio kwa timu pinzani na hilo ndilo tunahitaji. Tunapopoteza mpira anakuwa wa kwanza kuzuia mashambulizi.
 
"Ana sifa za uongozi na hilo ni wazi kabisa kulingana na anavyoshirikiana na wachezaji wengine. Hizi ni sifa tunazohitaji.”
 

Takwimu baina ya timu hizi

Mechi - 205
Arsenal - 81
Chelsea - 66
Sare - 58


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 07/22/2022