PAMOJA NA KUSINDA JANA ...BENCHIKHA ALIA NA UZEMBE WA CHE MALONE NA WENZAKE


KOCHA Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha amewakalia kooni mabeki wake kutokana na makosa yanayojirudia mara kwa mara kwa kuruhusu nyavu zao kutikiswa na mpinzani.
 
Amesema hafurahishwi na jinsi ya safu yake ya ulinzi na kuhakukisha anafanyia kazi haraka madhaifu ya kikosi cha timu hiyo kabla ya mechi zilizopo mbele yao ikiwemo Ligi Kuu Tanzania Bara na Michuano ya Kimataifa.
 
Kauli hiyo ni baada Simba kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKU FC ukiwa ni mchezo wa kwanza wa michuano ya Mapinduzi yanaendelea kufanyika visiwani Zanzibar.
 
kocha Benchikha amesema haukuwa mchezo rahisi kwao kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKU FC, ni mwanzo mzuri kupata ushindi muhimu kwao walihitaji kuanza mashindano.
 
Amesema wameshinda lakini hana furaha na uwezo ulioonyeshwa na safu yake ya ulinzi kutokana na makosa yaliyofanywa hali ya kuwa wana wachezaji wakubwa kwa kufanya makosa ya mara kwa mara.
 
“Makosa kama hayo hayavumiliki kuhakikisha tunafanyia kazi mapema kama wapinzani wetu wangekuwa makini huenda wangepata bao zaidi ya moja maana walifunga na wakapoteza nafasi nyingine mbili tumefanya makosa kama wangekuwa makini wangetuadhibu,” amesema Benchikha.
 
Amesema bado ana kazi kubwa katika safu ya ulinzi na kuifanyia kazi haraka na kusisitiza kuwa wanatakiwa kuwa makini katika mechi zijazo ili kutorudia makosa ambayo wanayafanya.
 
Akizungumzia kiwango cha nyota wake mpya, Salehe Karabaka alisema ameonyesha kiwango kizuri na kitendo cha kufunga kwenye mchezo wa kwanza kitamjenga.
 
“Unapocheza mchezo wa kwanza na kufunga baada ya dakika mbili ni jambo zuri nimefurahishwa nae na ana kesho iliyo bora na tuko hapa kwaajili ya kumsaidia kiufundi ili aweze kufika mbali,” amesema Benchikha.


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Bashiri popote
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway. 
 
 

Published: 01/12/2024