MOLOKO AONYESHWA MKONO WA KWA HERI YANGA....GAMONDI KABARIKI KIBOSI TU YANI


Hakimiliki ya picha: Soka la Bongo


WAKATI wa dirisha dogo la usajili linafungwa leo uongozi wa Yanga umeachana na winga wao, Jesus Moloko kwa makubali ya pande zote mbili.
 
Hatua hiyo ni baada ya nyota huyo hajawa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Kocha Miguel Gamondi ndani ya timu hiyo kutokana na ushindani wa namba.
 
Moloko alikuwa kwenye kikosi cha timu ya Yanga kilichoshiriki Mapinduzi
2024 kikagotea hatua ya robo fainali kwa kushuhudia ubao ukisoma Yanga
1-3 APR FC.
 
Raia huyo wa DR Congo ndani ya ligi hajapata zali la kufunga huku timu hiyo ikiwa imecheza jumla ya mechi 11 ikishinda 10 na kupoteza mchezo mmoja.
 
Kwa mujibu wa Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe wamechukuwa maamuzi ya kuachana na winga huyo kutokana na makubaliano ya pande zote mbili na kupisha nafasi ya usajili mpya kuingia.
 
Amesema wanamtakia kila la kheri nyota huyo anayokwenda na muda wowote kuanzaia sasa watatambulisha mshambuliaji mpya ambaye anakuja kukata kiu ya wananchi.
 
Kamwe anesema wamefanya mabadiliko machache kwa kufuata mapendekezo ya kocha Miguel Gamondi, ikiwemo kuimarisha safu ya ushambuliaji.
 
Amesema wamesikia kilio cha benchi la ufundi na mashabiki wa timu hiyo kuhakikisha katika usajili huu wanaimarisha safu ya ushambuliaji kwa kuleta mtu hatari.
 
“Ni kweli tumefanya kazi tuliyotumwa na kusikililiza kilio cha, kocha Gamondi pamoja na mashabiki wetu juu ya kusajili mshambuliaji tayari tumeshakamilisha usajili wake na atakuwa sehemu ya kikosi cha timu yetu kipindi chote cha mkataba wake,” amesema Kamwe.
 
ameeleza kuwa tayari kuna baadhi ya wachezaji wametolewa kwa mkopo kulingana na jinsi ya mapendekezo ya kocha Gamondi na kupisha usajili mpya kuimarisha katika nafasi chache.
 
Kamwe amesema hawakuwa na maboresho makubwa sana kwa sababu kikosi chao bado kipi inara na kuweza kuendelea walipoishia katika michezo iliyopo mbele yao ikiwemo ligi kuu Tanzania Bara, FA na Ligi ya Mabingwa Afrika.
 
MOLOKO HUYU HAPA.,
 
MUDA mchache baada ya  kuachwa kwa winga, Jesus Moloko na Yanga kwenye dirisha hili la usajili kupisha usajili mpya winga huyo amekiri hilo.
 
Yanga imeachana na winga huyo baada ya kuitumikia kwa misimu miwili hivyo ameungana na Wacongo wenzake Djuma Shaban, Yanick Bangala, Heritier Makambo, Chico Ushindi ambaye hakuweza kuendana na kasi ya Yanga na Fiston Mayele aliyeuzwa nje.
 
Akizungumza na kunukuliwa na gazeti la Mwanaspoti, Moloko alisema ni kweli amemalizana na Yanga na anatarajia kuondoka nchini kesho kwenda Congo kwa ajili ya maisha mengine mapya ya soka.
 
"Ni kweli nimepewa barua ya kuachana na Yanga na natarajia kwenda Congo kesho nawashukuru viongozi na mashabiki wa timu hii kwa maisha niliyoishi nao nikiwa ndani ya timu hiyo;
 
"Nilikuwa na misimu mitatu mizuri na Yanga nimeishi vizuri na wachezaji wenzangu, viongozi na hata mashabiki nawatakia kila la kheri kwenye mashindano wanayoshiriki ndani na nje," alisema

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Bashiri popote
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 01/16/2024