MAYELE:- TANZANIA WAKIKAZA ...ZAMBIA WATAKUFA GOLI NYINGI SANA


Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya DR Congo Fiston Kalala Mayele amesema Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ bado ina nafasi kubwa ya kusonga mbele katika michuano ya Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ inayoendelea nchini Ivory Coast.
 
Taifa Stars ilianza vibaya Michuano hiyo jana Jumatano (Januari 17) kwa kufungwa 3-0, dhidi ya Morocco katika mchezo wa Mzunguuko wa Kwanza wa Kundi F, uliopigwa kwenye Uwanja wa Laurent Pokou, mjini San-Pédro.
 
Mayele ambaye aliitumikia DR Congo katika mchezo dhidi ya Zambia na kuambulia sare ya 1-1, amesema wachezaji wa Tanzania wana nafasi kubwa ya kubadilika na kucheza kwa kujituma katika mchezo wa Mzunguuko wa Pili.
 
Amesema anaamini Taifa Stars ina nafasi kubwa ya kupambana dhidi ya Zambia mwishoni mwa juma hili, na endapo wachezaji wataamua kujitoa kwa asilimia zote, ushindi utapatikana na watajiweka katika mazingira mazuri.
 
“Kundi bado lipo wazi, Tanzania wana nafasi ya kuendelea mbele katika michuano hii, ninafahamu baadhi ya wachezaji wana uwezo mkubwa wa kucheza kwa kujitoa, wakifanya hivyo ninaamini wana uwezo wa kuifunga Zambia.”
 
“Katika Michuano hii kila timu ina nafasi ya kupambana na kupata ushindi, ndivyo ilivyo hata kwa Tanzania, kwa hiyo kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Morocco, isiwavunje moyo kwa kuona wameshaondolewa, wanapaswa kujitoa na kupambana kwa hali yote.” Amesema Mayele.
 
Wakati Tanzania ikitarajia kucheza dhidi ya Zambia Jumapili (Januari 21) katika mchezo wa Mzunguuko wa Pili wa Kundi F, DR Congo itakua na kibarua cha kuikabili Morocco, ambayo kwa sasa inaongoza msimamo wa Kundi hilo.


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Bashiri popote
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 01/19/2024