Hakimiliki ya picha: Getty Images
2023/24 English Premier League
Matchday 21
Manchester United v Tottenham Hotspur
Old Trafford
Manchester, England
Januari 14, Jumapili 2024
Muda: 7:30pm
Tottenham watakabiliana na Manchester United katika mechi ya ligi ugani Old Trafford mnamo Januari 14 siku ya Jumapili.
Spurs walipitia kipindi cha matokeo magumu kati ya Novemba 6 hadi Desemba 7 ambapo hawakushinda mechi hata moja na sasa wamefanikiwa kushinda mechi 4 kati ya mechi 5 za ligi zilizopita. Wanashikilia nafasi ya tano, alama moja nyuma ya wapinzani wao wa jadi Arsenal.
Vijana wa Ange Postecoglou walipata ushindi wa 3-1 dhidi ya Bournemouth 3-1 ugani Tottenham Hotspur Desemba 31 baada ya kupoteza 4-2 dhidi ya Brighton kwenye mchezo wa ligi siku tatu awali.
Spurs wapo alama tano mbele ya West Ham ambao walitoa sare ya 0-0 dhidi ya Brighton walioko nafasi ya saba Januari 2 huku Arsenal wakishuka hadi nafasi ya nne baada ya kupoteza mchezo wa pili wa ligi mfululizo.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
The Red Devils walipata ushindi mmoja tu katika mechi tano za mwezi Desemba na matarajio yao ni kufanya vizuri mwaka huu mpya.
United chini ya Erik ten Hag walimaliza mwaka kwa kupoteza 2-1 dhidi ya Nottingham Forest Desemba 30 na sasa wanashikilia nafasi ya 8, alama 9 chini ya nafasi yanne.
Alejandro Garnacho amepokea shutuma nyingi kuwa hafungi magoli kwa faida ya timu hiyo tangu kupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza lakini amejibu lawama hizo kwa kucheza vizuri katika mechi mbili zilizopita. Raia huyo wa Argentina alifunga magoli mawili dhidi ya Aston Villa Desemba 26 kabla ya kumuandalia pasi Marcus Rashford iliyozalisha goli la kusawazisha dhidi ya Forest.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Richarlison alifunga goli moja tu katika michezo 10 ya kwanza kabla ya kupata jeraha lakini sasa anaonekana kuwa katika hali nzuri. Raia huyo wa Brazil amefunga magoli matano katika mechi tano zilizopita.
Ten Hag amelaumu majeraha kuwa sababu ya matokeo yao duni msimu huu kwani hajafanikiwa kupanga kikosi chake bora mechi za kwanza 20.
"Hatujapata kupanga kikosi kimoja mfululizo. Tunalazimaka kupangua kikosi chetu mechi hadi mechi,” raia huyo wa Uholanzi aliambia Sky Sports.
"Inachangia kupangua na kuvuruga mbinu zetu na kupelekea matokeo mseto. Katika safu ya ulinzi tumechezesha wachezaji tisa tofauti. Hii sio sababu ya matokeo duni. Mashabiki wanahitaji kupata matokeo mazuri kutoka kwa timu yao. Hilo ni lengo letu.
"Majeraha yamekuwa kikwazo kikubwa. Kuna sababu nyingine lakini kubwa kuliko zote ni majeraha. Wachezaji wengi watarejea mwezi Januari na tunatarajia matokeo yataimarika.”
Postecoglou ameridhishwa na uchezaji wa timu yake msimu huu hata pale wanapopoteza mechi. Anazidi kushuhudia wachezaji wake wakiimarika siku hadi siku.
"Unapojaribu kufanikisha jambo lazima kutakuwa na changamoto. Nimeshuhudia wachezaji wangu wakiimarika. Sio kwenye matokeo tu bali kwa ujumla. Nimeshuhudia hilo leo.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Man United - 3
Tottenham - 1
Sare - 1
Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 21:
Januari 12, Ijumaa
10:45pm: Burnley v Luton Town
Januari 13, Jumamosi
3:30pm: Chelsea v Fulham
8:30pm: Newcastle United v Manchester City
Januari 14, Jumapili
5:00pm: Everton v Aston Villa
7:30pm: Manchester United v Tottenham Hotspur
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.